Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Kenyatta ateuwa jopo la watu 7 kuwahoji wagombea nafasi wazi katika IEBC

419f6a0157dc6e82 Rais Kenyatta ateuwa jopo la watu 7 kuwahoji wagombea nafasi wazi katika IEBC

Tue, 27 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Rais Uhuru Kenyatta katika taarifa ya gazeti la tarehe 16 Aprili, alitangaza nafasi nne katika IEBC kuwa wazi

- Nafasi hizo zilibaki wazi kufuatia kujiuzulu kwa makamishna Paul Kurgat, Margaret Mwachanya na Connie Maina mnamo Aprili 16, 2018

- Kamishna mwingine, Roselyne Akombe, pia aliondoka katika tume hiyo siku chache kabla ya kurudiwa kwa uchaguzi wa urais wa 2017

- Wajumbe wa jopo la uteuzi ni pamoja na Elizabeth Muli, Gideon Solonka, Awori James Achoka, Elizabeth Meyo, Dorothy Kimengech, Joseph Ngumbi Mutie na Faradim Suleiman Abdalla

Rais Uhuru Kenyatta ameteua jopo la watu saba litakalofanya kazi ya kuwahoji wagombea wa nafasi nne zilizo wazi katika Tume Uhuru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).

Katika ilani ya gazeti la Jumatatu, Aprili 26, kiongozi wa taifa aliteua wanachama wafuatao:

Elizabeth MuliGideon SolonkaAwori James AchokaElizabeth MeyoDorothy Jemator KimengechJoseph Ngumbi MutieFaradim Suleiman AbdallaWajumbe wa jopo hilo waliteuliwa kulingana na Sheria ya IEBC, ya 2020.

Jopo hilo la uteuzi ndani ya wiki moja linatarajiwa kuruhusu maombi kutoka kwa watu waliohitimu kuhojiwa kujaza nafasi zilizo wazi.

Majina ya wagombeaji watakaowasilisha maombi ya kazi yatachapishwa kwenye wavuti ya Tume ya Utumishi wa Umma na magazeti mawili yanayosomwa kitaifa.

Baadaye jopo hilo litazingatia maombi na wagombea walioteuliwa kulingana na sifa zao na uzoefu unaohitajika kwa kazi hiyo.

Nafasi za IEBCUhuru katika ilani ya gazeti la tarehe 16 Aprili, alitangaza nafasi nne katika IEBC kuwa wazi.

"Ninatangaza nafasi katika nafasi za wanachama wanne wa IEBC," alitangaza kulingana na Kifungu cha 7A (2) Sheria ya IEBC 2011.

Nafasi hizo zilibaki wazi kufuatia kujiuzulu kwa makamishna Paul Kurgat, Margaret Mwachanya na Connie Maina mnamo Aprili 16, 2018.

Watatu hao walijiuzulu kutoka IEBC wakitaja ukosefu wa imani kwa uongozi wa mwenyekiti wake, Wafula Chebukati.

"Kwa muda mrefu sana na kwa njia nyingi, mwenyekiti wa tume ameshindwa kuwa thabiti wa kuongoza meli katika nyakati ngumu na kutoa mwelekeo inapohitajika."

"Badala yake chini ya uongozi wa Chebukati, chumba cha bodi ya tume kimekuwa mahali pa kueneza habari potofu, sababu za kutokuaminiana na nafasi ya kugombana na kusaka sifa za mtu binafsi," walisema katika taarifa ya pamoja.

Kamishna mwingine, Roselyne Akombe, pia aliondoka katika tume hiyo siku chache kabla ya kurudiwa kwa uchaguzi wa urais wa 2017.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke