Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Kenyatta amvaa Waziri aliezuia mahindi mpakani "wewe nakupa wiki mbili" (+video)

Df2f5824 6d07 448f 9552 Aedb6d275eed 660x400.jpeg Rais Kenyatta amvaa Waziri aliezuia mahindi mpakani "wewe nakupa wiki mbili" (+video)

Wed, 5 May 2021 Chanzo: millardayo.com

Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta ametoa wiki mbili kwa ajili ya kushughulikiwa tatizo la mrundikano wa mahindi  katika eneo la mpakani ili biashara ziendelee kama awali.

“Mimi nitaje mambo mawili nayotaka yatendeke na hii ninataka yafanyike wiki hii na wiki ijayo, kwanza ni mawaziri ambao wanahusika muende mtatue msongamano ambao upo Taveta , Holili,  na pale Namanga magari yaweze kutembea, kama ni certificate za covid- 19 mawaziri wa afya wajue namna ya kufanya certificate ikitolewa Tanzania iwe sawa na aingie Kenya na vinginevyo”  Rais Kenyatta

“Pili ni mahindi ambayo yamelala mpakani, waziri mimi nakupatia wiki mbili mahindi yote yawe yamefunguliwa na maneno yaishe kwasababu hatutaki kuumiza watu wetu,”  Rais Kenyatta

Chanzo: millardayo.com