Rais Paul Kagame wa Rwanda amefanya mabadiliko kwenye baraza lake la Mawaziri na kumuondoa kazini bwana Johnston Busingye aliyehudumu kwa muda mrefu kwenye baraza hilo na sasa anakwenda kuwa Balozi wa Uingereza.
Nafasi ya Waziri wa Haki imeachwa wazi mpaka sasa baada ya kuondolewa kwa Busingye.
Balozi aliyekua nchini Uingereza sasa atarejea kuwa Waziri wa Madini, Gesi na Mafuta.
Bwana Busingye amekuwa waziri tangu mwaka 2013 na kabla ya hapo alikuwa Rais wa Mahakama Kuu ya Rwanda ikiwa ni kati ya kazi alizowahi kuzitumikia.
Kupitia ujumbe wake kwenye mtandao wa Twitter, Busingye amesema:
“Kwa unyenyekevu napenda kushukuru kwa maamuzi haya ya Rais mshehimiwa Paul Kagame kuniteua kuwa Balozi wa Rwanda nchini Uingereza. Naahidi nitafanya kila lililo ndani ya uwezo wangu kuipeleka Rwanda kwenye viwango vya juu sana.
Mabadiliko ya baraza la mawaziri pia yamewagusa mtendaji mkuu wa wizara ya Madini, Gesi na Mafuta, Francis Gatare, ambaye amepelekwa ofisi ya Rais ambapo atakua mshauri wa Rais kwenye masuala ya uchumi.