Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Julius wa Sierra Leone amechaguliwa tena kwa muhula wa pili

Rais Siera Leon Rais Julius wa Sierra Leone amechaguliwa tena kwa muhula wa pili

Wed, 28 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Julius Maada Bio amechaguliwa tena kuiongoza Sierra Leone kwa muhula wa pili kwa kuibuka na ushindi wa asilimia 56 ya kura zilizopigwa. Haya ni kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo.

Mshindani wake mkuu katika uchaguzi wa Rais Samura Kamara ameshika nafasi ya pili kwa kuibuka na asilimia 41.6 ya kura zilizopigwa. Hayo ni kwa mujibu wa matokeo ya mwisho ya uchaguzi yaliyotangazwa huko Freetownjana na Mohamed Kenewui Konneh Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya Sierra Leone.

Chama cha upinzani cha All People’s Congress (APC), kilikuwa kimepinga zoezi la kuhesabu kura ambacho ambapo juzi Jumatatu kiliilaumu Tume ya Uchaguzi kwa kutowashirikisha wawakilishi wa vyama vya upinzani katika zoezi hilo, kukosekana uwazi huku kikisema kuwa Tume ya Uchaguzi imeshindwa kuwajibika kuhusu suala hilo.

Chama cha upinzani cha APC ha huko Sierra Leone pia kimedai kukosekana kwa taarifa kuhusu vituo au wilaya ambazo kura za uchaguzi wa rais zilitoka. Kilisema kuwa hakitakubali matokeo bandia na ya udanganyifu ya uchaguzi wa Rais wa Sierra Leone.

Wakizungumza na waandishi wa habari juzi Jumatatu waangalizi wa uchaguzi wa Umoja wa Ulaya walisema kuwa kutokuwa wazi na kushindwa kuwasiliana Tume ya Uchaguzi ya Sierra Leone kumesababisha kutoaminiana katika mchakato mzima wa uchaguzi. Waangalizi hao walisemakuwa wameshuhudia ghasia katika vituo saba vya kupigia kura wakati wa uchaguzi na vinginevitatu wakati wa kufunga na katika marhala ya kuanza kuhesabu kura.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live