Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Daniel arap Moi afariki dunia

94324 Moi+pic Rais Daniel arap Moi afariki dunia

Tue, 4 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Nairobi. Rais wa zamani wa Kenya, Daniel arap Moi amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95.

Rais Uhuru Kenyatta ametangaza kifo hicho kilichotokea  usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Nairobi alikokuwa anapata matibabu.

Moi alizaliwa Septemba 2, mwaka 1924, katika jamii ya wakulima katika eneo la Baringo, magharibi mwa Kenya.

Jina lake la kwanza lilikuwa Toroiticha arap (mwana wa) Moi lakini baadaye akabatizwa katika Ukristo na kupewa jina la Daniel wakati huo akiwa mwanafunzi.

Moi aliyeshika uraia wa Kenya kati ya mwaka 1978 hadi 2002, alikuwa mmoja wa mwanasiasa mashuhuri waliofanikiwa, akitoka jamii ndogo ya Tugen, mojawapo ya makundi yanayounganisha kabila kubwa la Wakalenjin.

Alianza kufanya kazi kama mwalimu mwaka wa 1945 katika shule ya African Government School na mwaka mmoja baadaye akiwa na umri wa miaka 22 akateuliwa kuwa mwalimu mkuu.

Pia Soma

Advertisement
Machi 1957 Moi alikuwa mmoja wa watu weusi wanane waliochaguliwa kuwa wanachama wa Bunge la Ukoloni ambalo kwa kifupi lilifahamika kama LegCo.

Mapema mwaka 1960 alikuwa mmoja wa wajumbe walioteuliwa kuhudhuria mkutano katika Lancaster House jijini London, ambapo Katiba mpya iliandaliwa na kuwapa Waafrika viti vingi katika Bunge.

Mwaka 1961 aliteuliwa kuwa Waziri wa Elimu, na katika baraza la mawaziri la muungano wa vyama vya kisiasa vilivyoshirikisha Kanu (Kenya African National Union), Kadu (Kenya African Democratic Union - chama cha Moi) baadaye aliteuliwa kuwa Waziri wa Serikali za Mitaa.

Kenya baadaye ilipata Uhuru mwaka 1963 na Jomo Kenyatta akawa Waziri Mkuu, naye Moi akateuliwa kuwa Waziri kivuli wa kilimo katika muungano wa upinzani. Siasa za Kadu zilidorora kisha chama hicho kikavunjwa.

Viongozi wengi wa Kadu, akiwemo Moi, walijiunga na chama cha Kanu

Mwishoni mwa mwaka 1964, wakati Jomo Kenyatta alipotawazwa kuwa Rais, Moi aliapishwa kama Waziri wa mambo ya ndani.

Akiwa bado anashikilia Wizara hiyo mwaka 1967 aliteuliwa kuwa Makamu wa Rais na naibu mwenyekiti wa chama cha wabunge wa Kanu.

Kenyatta alipofariki dunia Agosti 1978, Moi aliyekuwa makamu wa Rais alichukua wadhifa wa kaimu Rais.

Mwezi Oktoba 1978 alichaguliwa kwa wingi wa kura kuongoza Kanu, chama pekee nchini Kenya wakati huo na pia alichaguliwa pia kuwa Rais wa Pili wa Kenya.

Agosti 1982 kulitokea jaribio la mapinduzi lakini lilizimwa na wanajeshi waaminifu kwake.

Baadaye mwezi huo Moi alivunja kikosi cha jeshi la wanaanga, ambao wengi wao waliongoza jaribio hilo la mapinduzi.

Tukio hilo kwa mujibu wa BBC lilimpa nafasi Moi kuimarisha madaraka yake kwa kuwatimua wote walioshiriki au kushukiwa kushiriki katika jaribio hilo.

Akiwa madarakani, miongoni mwa mabadiliko aliyofanya ni kurejesha vyama vingi vya kisiasa lakini akatumia ujanja wa kuyagawa makabila mbalimbali nchini na kushinda uchaguzi miaka ya 1992 na 1997.

Hata hivyo utawala wa Moi ulidumaa kiuchumi na Serikali yake ilishutumiwa kwa ufisadi na hivyo Shirika la Fedha duniani (IMF) na Benki ya dunia (WB) walikataa kutoa mikopo kwa Kenya.

Katika Uchaguzi wa 2002 Moi hakugombea kwa kuwa alikuwa anazuiwa kushiriki kikatiba, hata alipojaribu kumwachia nafasi hiyo Uhuru Kenyatta, alishindwa vibaya na huo ukawa ndio mwanzo wa mwisho wa chama cha Kanu.

Mwaka 2007 Rais Kibaki alimteua Rais Moi kuwa Balozi Maalumu wa Kenya nchini Sudan Kusini.

Mwaka 2010, wakati wa kampeni za kuidhinishwa kwa Katiba Mpya, Moi aliungana na wanasiasa kadhaa na viongozi wa makanisa kupinga katiba iliyopendekezwa.

Hata hivyo, upande wao ulishindwa kwenye kura ya maamuzi kuhusu katiba hiyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz