Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais DRC:  Magufuli alikuwa mkombozi uchumi wa Afrika

7b0ffbcc593e84a201fda6f4472a47fd.jpeg Rais DRC:  Magufuli alikuwa mkombozi uchumi wa Afrika

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Felix Tshisekedi ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa nchi za Afrika amesema kuwa Dk John Pombe Magufuli alikuwa kiongozi mwenye maono kwenye uchumi wa Afrika.

Rais Tshisekedi ameyasema hayo alipokuwa akitoa salamu za rambirambi leo Dodoma ambapo alisema Magufuli kuwa ameacha alama Afrika na kuna mengi ya kujifunza na kuyafanya ili kumuenzi.

Ameongeza pia Hayati Magufuli aliifanya Afrika iheshimike tena na pia ametimiza ndoto za waasisi wa nchi barani Afrika.

“Pumzika kwa Amani Magufuli, “ alimalizia Rais huyo wa DRC

Chanzo: www.habarileo.co.tz