Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Bouteflika wa Algeria Afariki Dunia

Rais Bouteflika Wa Algeria Afariki Rais wa zamani wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika.

Sat, 18 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa zamani wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 84 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Bouteflika aliongoza nchi hiyo kwa karibu miongo miwili na kuachia madaraka mwaka 2019 baada ya jaribio lake la kugombea muhula wa tano kusababisha maandamano makubwa. Alikuwa kiungo muhimu katika vita vya kupigania uhuru wa Algeria miaka ya 1950 na 60.

Mwaka 1999, baada ya Algeria kujikwamua kutoka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilisababisha vifo vya karibu watu 200,000, alikuwa raia baada ya kuombwa na jeshi la nchi hiyo.

Bouteflika hajaonekana hadharani tangu mwaka 2013, baada ya kuugua kiharusi ambacho kiliathiri uwezo wake wa kuzungumza na kutembea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live