Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Botswana: Magufuli alikuwa kiunganishi Afrika

Ebe17a10281473667563945e5fda697c.jpeg Rais Botswana: Magufuli alikuwa kiunganishi Afrika

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

RAIS wa Botswana, Mokgweetsi Masisi amesema aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli alikuwa na haiba ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere na atakumbukwa kwa michango yake katika kuiunganisha Afrika.

Rais Masisi ameyasema hayo leo katika viwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma, akitoa salamu zake za rambirambi kufuatia kifo cha Rais John Magufuli kilichotokea Machi 17 katika hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam.

Alisema Hayati Mwalimu Julius Nyerere alipendwa na watu wengi duniani hivyo Tanzania imeendelea kuondokewa na watu muhimu.

"Kwa kumuenzi hata sisi Botswana tumeanza kufundisha Kiswahili katika shule zetu kutokana na msimamo na msisitizo wake kwa lugha hiyo, hakika alikuwa mtu muhimu sana," amesema Masisi.

Kiongozi huyo amemtaka Rais Samia Suluhu Hassan kusimama imara bila kuogopa na Watanzania wamuunge mkono ili kuyaendeleza na kuyaenzi aliyoanzisha mtangulizi wake.

Amesema Bara la Afrika limempoteza mtu muhimu aliyekuwa bado mchango wake unahitajika kwa wakati huu katika masuala ya kiuchumi.

Amesema Botswana itaendelea kushirikiana kwa karibu na Tanzania kwa mambo mengi kutokana na mazuri aliyoanzisha na ndoto za Magufuli.

Chanzo: www.habarileo.co.tz