Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Biya wa Cameroon, Kagame wa Rwanda wabadili viongozi wa jeshi

Biya Kagame (600 X 338) Rais Biya wa Cameroon, Kagame wa Rwanda wabadili viongozi wa jeshi

Thu, 31 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchi za Rwanda na Cameroon zimefanya mabadiliko katika vikosi vya usalama na kijeshi.

Jana Jumatano Rais wa Cameroon Paul Biya mwenye umri wa miaka 90 alifanya mabadiliko makubwa katika wizara ya ulinzi ya nchi hiyo.

Miongoni mwa nyadhifa alizozifanyia mabadiliko ni pamoja na mjumbe wa kiti cha Urais anayeshughulikia ulinzi, wafanyakazi wa jeshi la anga, jeshi la wanamaji na polisi.

Biya aliyeingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka wa 1982, ni miongoni mwa marais waliokaa madarakani muda mrefu zaidi barani Afrika.

Nako nchini Rwanda, Rais Paul Kagame amewateua majenerali wapya pamoja na kuwapandisha vyeo vya kanali maofisa wapya vijana. Mbali na hayo Kagame aliidhinisha kustaafu kwa maofisa 83 wakuu wa kijeshi.

Kagame mwenye umri wa miaka 65 amekuwa madarakani tangu mwaka 2000 akiwa miongoni mwa marais waliokaa muda mrefu.

Mnamo 2015, katiba ya Rwanda ilibadilishwa ili kumruhusu Kagame kubaki rais hadi 2034.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Cable, maamuzi ya Kagame na Biya kubadilisha wanajeshi wao yanakuja siku chache baada ya wanajeshi kunyakua mamlaka nchini Gabon.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live