Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais: Algeria si tishio kwa mtu yeyote

Algeria Algeria Algeria si tishio kwa mtu yeyote

Mon, 26 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Abdelmajid Tebboune wa Algeria ametetea mamlaka ya kujitawala nchi yake na kubainisha kwamba, nchi hiyo si tishio kwa yeyote yule.

Rais wa Algeria amesema hayo katika hotuba yake kwenye luteka ya kijeshi iliyopewa jina la "Fajr 2023" iliyofanyika kusini mwa mji mkuu Algiers. Hii ni mara ya kwanza kwa luteka ya kijeshi nchini Algeria kufanyika chini ya uangalizi wa Rais wa nchi kwani kabla ya hapo luteka za kijeshi zimekuwa zikifanyika chini ya usimamizi wa mkuu wa majeshi.

Akihutubia katika maonyesho hayo ya kijeshi, Rais Abdelmajid Tebboune amesisitiza kwamba, Algeria imekuwa na itaendelea kuwa ngome ya amani na usalama na kwamba, taifa hilo tangu lilipojipatia uhuru na mamlaka yake ya kujitawala haijawahi kuwa chanzo cha tishio na hujuma dhidi ya mtu yeyote.

Gazeti la al-Quds al-Arabi limemnukuu Rais Tebboune akieza kwamba, ni jambo lililo wazi kwa kila mtu ya kwamba, kujipatia mambo ya kujiimarisha ni moja ya vipaumbele vyetu kwa ajili ya kulinda mamlaka ya kujitawala mbele ya njama na vitisho dhidi ya amani na uthabiti wa eneo.

Itakumbuukwa kuwa, Algeria na Morocco zimekuwa na mzozo wa muda mrefu baina yao ambao umekuwa ukitishia pakubwa maelewano baina yao.

Mnamo Agosti 24, 2021, Algeria ilitangaza kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Morocco kwa sababu ya "kuchukuliwa hatua za kiuhasama" na Rabat. Hata hivyo Morocco ilisema, hatua zinazodaiwa kuchukuliwa na nchi hiyo ni "visingizio hewa na visivyo na msingi". Suala la hatima ya Sahara Magharibi kati ya eneo hilo kuunganishwa na kuwa sehemu ya ardhi ya Morocco au kuwa taifa huru linalojitawala kikamilifu ndio sababu kuu ya mzozo wa kihistoria kati ya Algeria na Morocco.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live