Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Akufo-Addo aongoza uchaguzi Ghana

32d96116160f8b2d6987f778d9a15ff5 Rais Akufo-Addo aongoza uchaguzi Ghana

Wed, 9 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

BADO kura zinaendelea kuhesabiwa nchini Ghana baada ya Uchaguzi Mkuu wa rais na wabunge kufanyika juzi kwa amani.

Hadi jana asubuhi, matokeo ya awali yalikuwa yanaonesha Rais wa Ghana anayetetea nafasi hiyo, Nana Akufo-Addo, anaongoza dhidi ya mpinzani wake John Mahama ambaye ni rais mstaafu wa taifa hilo.

Aidha, chama tawala cha National Patriotic Party (NPP) kimeonekana pia kuongoza katika viti vya ubunge ingawa chama pinzani cha National Democratic Congress (NDC) kinazipinga taarifa hizo.

Uchaguzi nchini humo ulifanyika juzi kwa amani ingawa baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwepo kwa kundi lililorusha risasi katika kituo kimoja cha kupigia kura na kujeruhi watu wawili.

Jumla ya watu milioni 17 walijiandikisha kupiga kura. Katika nafasi ya urais, wagombea 11 waliwania nafasi hiyo akiwemo Rais Akufo-Addo, anayetetea kipindi chake cha awamu ya pili.

Wakati wa kampeni, masuala kadhaa yalijitokeza ikiwemo suala la ajira kwa vijana, masuala ya usalama, na athari za covid 19 kwa uchumi wa nchi hiyo.

Chanzo: habarileo.co.tz