Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Aidhinisha Waziri Mkuu Kujiuzulu

Burkinaaa Rais Aidhinisha Waziri Mkuu Kujiuzulu

Thu, 9 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

RAIS wa Burkina Faso Roch Marc Christian Kabore amekubali kujizulu kwa Waziri Mkuu Christophe Dabire na serikali yake. Kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Dabire, kumetangazwa kupitia Televisheni ya taifa na Katibu Mkuu wa serikali Wenceslas Sanou.

Kwa mujibu wa sheria ya Burkina Faso, Waziri Mkuu akijiuzulu, anaondoka na Baraza lote la Waziri. Kwa sasa serikali nchini humo itasalia kwa uangalizi maalum hadi pale serikali mpya itakapoundwa.

Ripoti zinasema kuwa sababu kubwa ya kujizulu kwa Dabire, ni kufuatia kuendelea kuzorota kwa hali ya usalma nchini humo katika siku za hivi karibuni. Tangu mwaka 2015 makundi ya kijihadi yamewauwa watu zaidi ya Elfu mbili na wengine zaidi ya Milioni Moja na Laki nne, kuyakimbia makawao.

Mwezi Novemba watu 57 wakiwemo maafisa wa usalama wa akiba wapatao 53 waliuawa baada ya kushambuliwa na watu weNye silaha, Kaskazini mwa nchi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live