Mon, 16 May 2022
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Wabunge Nchini Somalia wamemchagua Hassan Sheikh Mohamud aliyekuwa Rais kati ya mwaka 2012 - 2017 kuongoza Taifa hilo.
Amepigiwa Kura 214, huku Rais Mohamed Abdullahi Mohamed aliyekuwa anawania Muhula mwingine akipata Kura 110.
Rais Mohamed amekubali matokeo ya Uchaguzi na Mohamud ameapishwa kuongoza Nchi hiyo ambayo Hali yake ya Kisiasa imekuwa tete kwa muda sasa.
Somalia imekosa Serikali Kuu yenye nguvu tangu kuondolewa kwa Mohamed Siad Barre mwaka 1991.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live