Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raila hawezi kubaliki Mt Kenya, Gavana Mutua amwambia Rais Uhuru

10d3c5531becd3b7 Raila hawezi kubaliki Mt Kenya, Gavana Mutua amwambia Rais Uhuru

Fri, 23 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mutua alisema ana familia Mt Kenya na anajua kumuuza Raila huko ni ngumu sana kutokana na dhana ya wakazi kumhusuAlisema kwa sasa ni lazima Rais atafute mbinu kabambe ya kukabilia ufuasi wa DP Ruto eneo hiloIwapo hilo halitafanyika Mutua alisema Kenyatta akubali kuwa DP atamrithi Ikulu 2022Gavana Alfred Mutua amemshauri Rais Uhuru Kenyatta kutafuta mbinu murwa kuhakikisha kuwa naibu wake William Ruto hana uungwaji mkono eneo la Mt Kenya.

Akiongea kwenye mahojiano Alhamisi na runinga ya Citizen Julai 22, Mutua alisema kwa sasa DP Ruto ana ufuasi mkubwa Mt Kenya.

Alisema mbinu ya Rais ya kujaribu kumuuza kinara wa ODM katika Mt Kenya haitafaulu kwani wakazi wa eneo hilo wana dhana mbaya kumhusu.

"Hatafaulu kumuuza Raila katika eneo la Mt Kenya kwa wakati huu. Na mimi ninaongea kama mtu ambaye yuko na jamaa eneo hilo na pia nina mizizi huko.



Read also

Mt Kenya Wamepoteza Mwelekeo Kisiasa, Gavana Joho Asema



Alisema Rais asipotafuta mbinu mufti ya kukabili DP katika eneo la Mt Kenya, basi atakuwa amewacha barabara wazi kwa Ruto kuchukua usukani 2022.

Hilo halitafaulu kwa asilimia mia moja. Ni lazima atafute mbinu nyingine iwapo anataka DP Ruto asipate kura kutoka eneo hilo ili asifaulu kumrithi," aliongeza Mutua.

Kulingana na Mutua, DP amekuwa mjanja na hutumia asasi za serikali kujitafutia umaarufu katika eneo hilo.



“DP Ruto amekuwa akichukua kura za Mt Kenya kwa kutumia viongozi wa humo na matunda ya mamlaka anayoshikilia.

Kama Rais hataki arithiwe na Ruto basi ni lazima atafute mpango mwingine, la sivyo basi akubali amrithi," aliongeza gavana huyo.

Umaarufu wa DP katika eneo la Mt Kenya umekuwa ukionekana kupanda huku wandani wake wakishinda kwenye chaguzi ndogo zilizofanyika.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.



Read also

Magazeti Jumatano, Julai 21: Kilonzo Adai Uhuru Anachezea NASA Shere

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke