Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raila azidi kuivuruga kambi ya Ruto

Be85c3b015325731 Raila azidi kuivuruga kambi ya Ruto

Sat, 16 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Uasin Gishu ni ngome ya kisiasa ya DP Ruto ambaye ni hasimu wake mkuu katika kinyang'anyiro cha kuingia Ikulu 2022 Kinara wa ODM Raila Odinga ametikisa ngome ya kisiasa ya hasimu wake William Ruto wakati wa ziara ya kupigia debe vuguvugu lake la Azimio la Umoja.

Wakazi walifurika mjini Edoret katika barabra ya Uganda na kumtaka Raila kuwahutubiaRaila licha ya kuwa hakuandamana na kigogo yeyote wa kisiasa eneo hilo alionekana kuwavutia wakazi hao.

Raila alipewa makaribisho ya heshima huku wakazi wakifurika mjini Eldoret kumpokea kwa furaha.

Ilikuwa ni wakati mgumu kwa Raila na msafara wake kupenya katika barabara ya Uganda kutokana na umati mkubwa uliokuwepo.

Nje ya jengo la Sacred Heart of Jesus Cathedral wakazi walimtaka Baba kuwahutubia na hivyo akalazimika kufanya hivyo.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke