Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raila aunga mkono uamuzi wa makanisa kupiga marufuku siasa madhabauni

0fgjhs59j561n8k7d Raila aunga mkono uamuzi wa makanisa kupiga marufuku siasa madhabauni

Thu, 16 Sep 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Kiongozi wa chama cha ODM, Raila Odinga ameunga mkono hatua ya makanisa kupiga marufuku kampeni za kisiasa madhabauni.

Raila Odinga alisema kanisa ni mahali pa kuabudu na hivyo siasa zinatakiwa kupigwa njeKiongozi huyo wa chama cha ODM alishukuru kanisa kuteta ukweli na usawa kwa kuwakosoa wanasiasa wanaotumia makanisa vibaya.

Matamshi yake yanakujia baada ya maaskofu wa Katoliki kujiunga na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kianglikana Jackson Ole Sapit kupiga marufuku siasa makanisani

Raila apinga siasa makanisaniRaila Odinga alisema kanisa ni mahali pa kuabudu na hivyo siasa zinatakiwa kupigwa nje ya kanisa.

“Ninatoa shukrani kubwa kwa makanisa kwa kushikilia ukweli na usawa na ninamuunga mkono askofu mkuu kwa hili. Kanisa halitakani kuwa mahali pa kupiga siasa. Matamshi ya siasa yanatakiwa kutolewa nje ya kanisa,’’ alisema.

Waziri mkuu huyo wa zamani alikuwa akizugumza Jumatano, Septemba 16, katika eneo la Ngecha, Limuru wakati wa mazishi ya Grace Muthoni, ambaye ni dada yake George Gichini, mwakilishi wa ODM katika kaunti ya Kiambu.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke