Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raila atangaza nia ya kuwania Urais Kenya 2022

23197ccd966f4c3c Raila atangaza nia ya kuwania Urais Kenya 2022

Sun, 22 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Akizungumza eneo la Bondo, Raila Odinga alisema yuko tayari kumenyana na Naibu Rais William Ruto mwaka 2022 Raila aliwaomba wafuasi wake kujitokeza kwa wingi kujisajili kupiga kura kuelekea chaguzi hizo zinazosubiriwa kwa hamu na ghamuTangazo la Raila linazima fununu ya iwapo atakuwa kwenye debe au laKiongozi wa ODM, Raila Odinga ametangaza rasma kuwa atajitosa kwenye mbio za kumrithi Rais Uhuru Kenyatta katika Uchaguzi Mkuu wa 2022.

Tangazo la waziri mkuu huyo wa zamani linakujia baada ya Mahakama ya Rufaa kuzika mswada wa Mpango wa Maridhiano(BBI).

Akizungumza eneo la Bondo, Raila Odinga alisema yuko tayari kumenyana na Naibu Rais William Ruto ambaye pia anamezea mate kiti hicho.

"Kwa miezi kadhaa, nimekuwa nikiskia watu wengine wakipiga kelele sana kuhusu wilibaro (akitaja mpango wa Ruto). Walikuwa na muda wa kupiga kelele, lakini sasa wakati umefika wa kuingia uwanjani kumenyana," alisema Raila.

Wakati wa hotuba yake, aliweka bayana kuwa BBI, ambayo ilikuwa inalenga kubadilisha katiba ya mwaka 2010, sasa ni mambo yaliyopita na fikra zake zinalenga kutwaa mamlaka.



Fauka ya hayo, Raila aliwaomba wafuasi wake kujitokeza kwa wingi kujisajili kupiga kura kuelekea ambayo imeratibiwa kuandaliwa Agosti 9, 2022.

Tangazo la Raila linazima fununu ya iwapo atakuwa kwenye debe au la kufuatia presha ya wafuasi wake.

Asonga mbele baada ya BBIRaila alisema yeye na mrengo wake wa ODM wameamua 'kuendelea na maisha' na maisha baada ya uamuzi wa mahakama kuwa BBI ni haramu.

Kwenye taarifa, Raila alisema imefika wakati kila upande uliohusika kuamua hatua watakayochukua baada ya uamuzi wa Ijumaa Agosti 20.

"Sisi, kama tulivyosema hapo awali, tulikuwa tujihusishe kiasi cha haja. Lakini sasa tunahisi kuwa itabidi tuendelee na mengine," Raila alisema.

Alisema ni wazi kuwa masaibu ni mengi Kenya na kwa hivyo atatafuta njia mbadala za kutatua masuala yaliyokuwa yameangaziwa na BBI.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke