Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raila apokea cha pili ya COVID-19, awashauri Wakenya kuchanjwa

Abd4cae0e9418cd1 Raila apokea cha pili ya COVID-19, awashauri Wakenya kuchanjwa

Wed, 22 Sep 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga alipokea chanjo hiyo Jumatano, Septemba 22 Raila aliwahimiza Wakenya kupata chanjo dhidi ya virusi hivyo hatari akisema ugonjwa huo ni kweli upoWaziri Mkuu wa zamani alipokea chanjo ya kwanza mnamo Julai 20, 2021, baada ya kunaswa na COVID-19 Kinara wa chama cha Orange Democratic Movement amepokea chanjo yake ya pili ya virusi vya COVID-19.

Taarifa kupitia chama chake cha ODM ilionyesha Raila alipokea chanjo hiyo Jumatano, Septemba 22, akiwataka Wakenya kupata chanjo dhidi ya virusi hivyo hatari.

"Chanjo ya pili na ya mwisho kwa baba ... Wacha tupate chanjo. Ni kweli COVID-19 ipo," alisema.

Waziri mkuu huyo wa zamani alipokea chanjo yake ya kwanza mnamo Julai 20, 2021.

Hii ilikuwa baada ya kupimwa na kupatikana na virusi vya ugonjwa wa COVID-19 siku chache baada ya kulazwa katika Hospitali ya Nairobi.

"Baada ya kuwa mwathiriwa wa virusi hivi hatari ninawahimiza wale wote ambao wanastahili kupata chanjo kupata chanjo," alisema.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke