Seneta wa Nandi Cherargei Samson sasa amesema ni dhahiri kwamba Kiongozi wa Chama cha ODM Mhe Raila Odinga ana njaa na kiu ya mamlaka kabla ya uchaguzi mkuu ujao wa 2027 hadi anaajiri umati.
Katika ujumbe wake kwenye Twitter, Mhe Cherargei alitoa maoni kwamba Wafadhili wa Raila wanajulikana sana na kwamba watawataja wachache siku zijazo.
Aidha, seneta huyo amekiri kuwa Raila atakamatwa kwani hayuko juu ya sheria.
"Wachache wa umati wa watu waliokodiwa wakimfuata Tinga. Tinga ana njaa ya mamlaka hiyo hajali & anaweza kukatiza Wakenya wa kawaida wanaojaribu kujikimu kimaisha. Uzururaji huu wa hadharani unakusudiwa kuhujumu uchumi na Tinga.
Relax Tinga HAYUPO juu ya sheria atakamatwa isipokuwa marafiki wa Azimio-OKA watasema yuko juu ya sheria!.
Wafadhili wa Tinga/Azimio-OKA wanajulikana tutawataja pamoja na baadhi ya NGOs kwa nia ya kuyumbisha serikali."
Wiki jana wakati wa maandamano ya saba saba, yaliyosababisha kukamatwa kwa baadhi ya waandamanaji na wengine kujeruhiwa, Cherargei alisema kwamba Raila anapaswa kukamatwa.
Haya yanajiri baada ya kinara huyo wa ODM kufanya mkutano wa ghafla siku ya Jumatatu katikati mwa mji siku ya Jumatatu.
Katibu mkuu wa UDA Malala kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter siku ya Jumatatu pia alimkejeli Raila kwa kuabiri matatu kuenda kazini.
Malala alihoji ni kazi gani kinara huyo na waziri huyo mkuu wa zamani alikuwa anaenda.
Cherargei na baadhi ya viongozi wa UDA wamekuwa wakosoajin wakubwa wa kinara huyo, kwa kupinga serikali ya Ruto.