Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raila amtetea Rais Uhuru Kenyatta kuhusu akaunti za mabilioni Ulaya

Bbb87e1e7271c6f3 Raila amtetea Rais Uhuru Kenyatta kuhusu akaunti za mabilioni Ulaya

Wed, 6 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Raila amesema yeye hana chochote kwenye akaunti za ughaibuni baada ya ufichuzi wa Pandora Papers lakini amemtetea Rais Kenyatta na familia yake akisema hakuna makosa yoyote kwa mtu kumiliki mabilioni ughaibuni.

Raila amesema muhimu ni mtu kuelezea jinsi alivyopata mabilioni anayomiliki na kuwekeza katika akaunti hizo. Kinara wa ODM Raila Odinga amesema yeye hana pesa kwenye akaunti za Ulaya kama viongozi wengine waliofichuliwa na upekuzi wa Pandora.

Akiongea na redio ya Chamgei Jumatano asubuhi, Raila amesema hakuna Sheria iliyovunjwa kwa mtu kuwa na akaunti nje ya Kenya.

"Mimi sina chochote huko nje, yangu iko Kenyaā€¯ alisema kiongozi huyo wa upinzani.

"Sioni kama kuna shida kuwa na accounts kwenye nchi za kigeni ijapokuwa kama ilikuwa ni ya ufisadi. Ijulikane pesa ambazo zimeingia huko zinatoka wapi," Raila aliongeza.

Alisema muhimu ni walio na akaunti hizo kuelezea jinsi walipata mabilioni hayo yaliyoweka majuu.

Ufichuzi wa Pandora umezua hisia mseto haswa baada ya familia ya Rais Uhuru Kenyatta kuhusiahwa na akaunti kadhaa zinazoripotiwa kuwa na mabilioni.

Wakosoaji wa Rais wamesema ufichuzi huo ni ishara ya mali yaliyoporwa Kenya na kufichwa katika akaunti hizo za Ulaya.

Hata hivyo, Raila amewataka Wakenya kutompaka tope Kenyatta na familia yake na badala yake kisibiri arejee nchini Ili kutoa taarifa zaidi kama alivyoahidi.

"Hakuna shida kuwa na account kule nje bora unaweza kusema jinsi ulifungua account. Vile Uhuru amesema atasema zaidi atakapo rudi," alisema

Ripoti hizo za Pandora zilichipuka Kenyatta akiwa ziarani ughaibuni lakini zilimfikia na kuahidi kuweka mambo wazi akirudi nchini.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke