Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raila amjibu Ruto baada ya vurugu "Mimi Sitaki Mambo ya Porojo"

D6503056b80cde97 Raila amjibu Ruto baada ya vurugu "Mimi Sitaki Mambo ya Porojo"

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Kinara wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) Raila Odinga, amejitenga pamoja na chama chake kuhusika katika vurugu vilivyoshuhudiwa wakati wa ziara ya Naibu Rais William Ruto eneo la Kondele mnamo Jumatano, Novemba 10.

Raila amesema kuwa Ruto, kama Mkenya mwingine yeyote yuko huru kutembea katika eneo lolote nchini na kuuza sera zake kwa wapiga kura. Waziri mkuu wa zamani alisema kuwa hataki kushirikishwa na porojoKauli ya Raila inakujia baada ya Ruto kumlaumu kwa vurugu hiyo akidai kuwa ndiye aliwatuma vijana kurushia msafara wake mawe.

Raila alisema kuwa Ruto, kama Mkenya mwingine yeyote yuko huru kutembea katika eneo lolote nchini na kuuza sera zake kwa wapiga kura.

Katika mahojiano na kituo cha Musyi FM mnamo Alhamisi, Novemba 11, waziri mkuu wa zamani alisema kuwa hataki kushirikishwa na porojo.

"Mimi sitaki kuingia kwa mambo ya porojo, labda niongee kwa mambo ya ukweli, Ruto ni Mkenya na anaruhusiwa kutembea popote kuuza sera zake," Raila said.

Atetea ODMKigogo huyo wa siasa alisema kuwa kabla ya ziara ya Ruto eneo hilo, chama cha ODM tawi la Kisumu kilikuwa kimetoa taarifa na kusema Naibu Rais yuko huru kupiga kampeni zake na kutangamana na wakazi.

"Chama chetu, tawi ya Kisumu kiilitoa taarifa kikasema Ruto Ruto kuuza sera zake kama mtu yeyote, kusiwe na vurugu yoyote," Raila aliongeza.

Raila alijitenga na vurugu hivyo akidai kuwa yeye pamoja na chama chake hawakuhusika.

"Mimi sio mtoto mdogo niende nitume watu warushie Ruto mawe, kwa sababu gani? Ruto ni kitu kidogo sana kwangu."

"Yeye anaweza kwenda Kisumu kila mahali vile anavyo tanga tanga kila mahali akipiga .. anabweka hapa na pale, ni haki yake, ni binadamu, apige kifua yake, akohoe, ateme mate, hio ni sawa kabisa, hio ndio mambo ya siasa nchi yetu," alisema Raila.

Ruto amlaumu Raila kwa vurugu ya KondoleKauli ya Raila inakujia saa chache baada ya Ruto Jumatano, Novemba 10, kumlaumu kwa vurugu hiyo akidai kuwa ndiye aliwatuma vijana kurushia msafara wake mawe.

"Ninamwomba rafiki yangu, kiongozi wa ODM, tafadhali, tusiwatumie watoto wetu kurusha mawe na kusababisha vurugu," Ruto aliandika kwenye Twitter.

Ruto alimwambia Raila kuwa badala ya kuwatumia vijana kurusha mawe, serikali yake kupiia mfumo wa uchumi wa Bottom-Up utabuni nafasi za kazi kwa vijana hao.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke