Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raila akiwaendesha marafiki kwenye gari la kifahari, adai kupenda chips vumbi

19698167b4fdf570 Raila awaendesha marafiki kwenye gari la kifahari, adai kupenda chips vumbi

Sun, 9 Jan 2022 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mgombea Urais kupitia ODM ya Kenya, Raila Odinga amewaendesha baadhi ya marafiki zake mtaani Karen katika gari lake la kifahari na kufurahia muda wake pamoja nao.

Wakati wa ziara hiyo, mwanasiasa huyo alijibu baadhi ya maswali kumhusu na chaguzi za Agosti Alionyesha matumaini kuwa atashinda uchaguzi wa Urais ambapo atamenyana na Naibu Rais William Ruto

Katika video iliyopakiwa kwenye kurasa zake za mtandao wa kijamii, Raila na diwani huyo walizungumzia mtaji wa KSh 6,000 ambazo aliwaahidi Wakenya wasioukuwa na ajira ikilinganishwa na mfumo wa uchumi wa bottom-up unapigiwa debe na Naibu Rais na William Ruto.

"Jambo la mikokoteni halina maana; pia sielewi uchumi wa chini kwenda juu," alisema.

Akionyesha matumaini kuwa atashinda uchaguzi wa urais, Raila alisema atashughulikia masuala yote ya Wakenya kwa jumla.

Kinara huyo wa upinzani pia alisema mke wake Ida anapenda maua.

Raila pia alifichua kwamba kila anapozuru Dagoretti, anapenda kula githeri, nyama choma na vibanzi vya mitaani almaarufu chips mwitu.

Kiongozi huyo alonekana kufurahia akipakia video hiyo kwenye Twitter akisema.

"Kufurahia na kuendesha gari hadi 2022 na marafiki wengine wapya. Labda katika maisha mengine, ningeweza kuwa dereva wa teksi."

Raila atimia umri wa miaka 77Haya yanajiri siku chache baada yake kuandaa bonge la karamu kwenye ukumbi wa Bomas of Kenya akiadhimisha bathdei yake ya 77.

Wakazi wa mjini Kisii na Homa Bay wakianika keki yake mitaani wakiungana naye kusherehekea hatua alizopiga.

Katika kaunti ya Nairobi, wakazi katika kati kati mwa jiji (CBD) waliandaliwa chai na keki.

Hasimu wake mkubwa kisiasa Ruto pia alimpamba na ujumbe mtamu siku hiyo akimtakia heri njema.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke