Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raila ahuzunishwa na wapenzi wanaoangamiza maisha ya wenzao

4ed1c5c05a003792 Raila ahuzunishwa na wapenzi wanaoangamiza maisha ya wenzao

Tue, 20 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Kiongozi wa Chama cha Orange Democratic Movement (ODM), Raila Odinga amezua wasiwasi kuhusiana na visa vya dhuluma ya kijinsia kuongezeka nchini.

Raila alisikitishwa na baadhi ya wapenzi ambao badala ya kukuza penzi lao hugeuka na kuwaua wenzao.

Kupitia kitandazi chake cha Twitter siku ya Jumanne, Aprili 20, Raila alisema endapo wapenzi wanashindwa kutatua tofauti zao, ni vyema kutengana na kuachia wenzao uhai wao.

"Ni jambo la kusikitisha kuwa baada ya kuteka moyo wa mwenzako, badala ya kuwapenda na kuwaenzi, baadhi hugeuka kuwa vita na wakati mwingine kifo. Endapo hamuwezi kusameheana, basi tenganeni na muwache uhai," Raila.

Raila alisema taifa hili linahitaji mjadala wa haraka kuhusu dhuluma ya kjinsia ili kumaliza visa hivi.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke