Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raila afanya kikao na Oparanya, Orengo licha ya madai ya ODM kuparaganyika

Abdeb792e64ba976 Raila afanya kikao na Oparanya, Orengo licha ya madai ya ODM kuparaganyika

Tue, 11 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Viongozi hao walikutana na Raila huku kukiwa na dhana kwamba walikuwa wakipanga kujiondoa kutoka ODM

- Oparanya na Orengo waliripotiwa kukutana Jumapili, na kuwaacha wafuasi wao katika hali ngumu kutokana na kwamba hawakumjulisha mtu yeyote juu ya mkutano wao

- Mkutano wao na Raila leo umeonekana kama dawa ya kutuliza maumivu miongoni mwa wafuasi wao

Katika hali ya kuondoa shaka, wanaodaiwa kuwa waasi katika chama cha Orange Democratic Movement (ODM) waliungana tena na kiongozi wa chama hicho Raila Odinga nyumbani kwake Karen Jumatatu, Mei 10.

Hii ilitokea wakati manung'uniko yakiwapo kwamba ODM kilikuwa kimetikiswa na mizozo ya ndani inayogonganisha vikundi viwili.

Seneta wa Siaya James Orengo na Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya waliripotiwa kukutana Jumapili, Mei 9, kujadili msimamo wao kuhusu yalitokea ambayo hatimaye yalizua mgogoro katika chama hicho.

Mbunge wa Rarieda Otiende Amollo pia alikuwepo wakati wa mkutano huo.

Oparanya ameonekana hivi karibuni kutofautina na kiongozi wa chama cha chungwa, mara nyingi akishirikiana na Naibu Rais William Ruto, na hivyo kusababisha hali ya kuwapo kwa mdaia kumhusu.

Wanachama ndani ya chama hicho walikuwa wamegawanywa kwenye mswada wa BBI, na kikundi kimoja kilishinikiza marekebisho kadhaa kufanywa kabla ya kupitishwa, huku kundi lingine likipinga na kushinisha mswada huo kupitishwa na mabunge yote jinsi ulivyo.

Kikundi kilichokuwa kikishinikiza marekebisho kiliongozwa na seneta Orengo ambaye aliungana na Otiende Amollo, katika kupambana na kundi lililokuwa likiongozwa na John Mbadii na Junet Mohammed, ambao walishikilia msimamo wa chama kuwa mswada upitishwe bila mabadiliko yoyote.

Hoja hizo zilisababisha kuondolewa kwa Otiende Amollo kutoka wadhifa wa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Maswala ya Bunge (JLAC), huku uvumi ukizidi kuwa Orengo pia alitazamiwa kuondolewa kutoka Uongozi wa Wachache katika Seneti.

Viongozi waliokutana na Raila wameonekana kama hatua ya kupunguza mvutano kati ya wafuasi wa ODM na vyama vingine vinavyohusika.

Muda mfupi baada ya kukutana na Raila, viongozi hao watatu walifululizia Kajiado, ambapo walikutana na Katibu Mkuu wa COTU Francis Atwoli nyumbani kwake.

Ingawa walisema mkutano na Atwoli ulikuwa wa kujuliana hali tu, wadadisi wa masuala ya siasa wametoa maoini tofauti, ikizingatiwa kiongozi huyo wa COTU amekuwa akiwapokea wanasiasa wazito wa humu nchini.

Viongozi wengine waliowahi kukaribishwa nyumbani kwa Atwoli ni Makamu Mwenyekiti wa Jubilee David Murathe, mgombea wa zamani wa ugavana Nairobi Peter Kenneth, kiongozi wa KANU Gideon Moi na Raila Odinga.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690. Tazama habari kemekem za TUKO hapa
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke