Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raila aapa kuwafunga jela waporaji wa fedha za umma akiingia madarakani

7e0ae5e80703bb46 Raila aapa kuwafunga jela waporaji wa fedha za umma akiingia madarakani

Sun, 7 Nov 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Raila ni mmoja wa wawaniaji wa urais wanaotaka kumrithi Rais Uhuru Kenyatta katika Uchaguzi Mkuu wa 2022 Alisimama katika vituo mbali mbali vya kaunti ya Nyandarua mnamo Jumamosi, Novemba 6, ambapo alipigia debe Azimio la UmojaKiongozi wa chama cha ODM alidhihirisha imani kwamba mapinduzi ya tatu yalifanyika haraka chini ya Azimio la Umoja Aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga amewapa notisi waporaji wa pesa za umma akisema arobaini zao zinakaribia.

Akizungumza katika vituo mbalimbali kaunti ya Nyandarua Jumamosi, Novemba 6, kiongozi huyo wa Orange Democratic Movement (ODM) alisema walioiba rasilimali za umma wana wasiwasi.

Daily Nation inaripoti kuwa Raila alidhihirisha imani kwamba mapinduzi ya tatu yalifanyika haraka chini ya Azimio la Umoja.

Raila, mmoja wa wawaniaji urais wanaotaka kumrithi Rais Uhuru Kenyatta katika Uchaguzi Mkuu wa 2022, alisema ni wezi wa rasilimali za umma pekee wanaotilia shaka uwezekano wa malipo ya KSh 6,000 kwa familia maskini.

"Kenya ina rasilimali nyingi. Sisi ni matajiri sana lakini rasilimali zetu zinaishia kwenye mifuko ya majambazi, ndio maana wameingiwa na hofu na kutilia shaka ninapoahidi malipo," alisema Raila.

Alisema hamna Mkenya aliyechagua kabila lake au eneo la kuzaliwa, na Azimio la Umoja litahakikisha usalama wa Wakenya wote bila kujali kabila na dini.

"Hamna Mkenya anayefaa kudhulumiwa, kutishiwa wala kubaguliwa kwa misingi ya kabila au dini," Raila alisema.

Aliahidi kumshirikisha Uhuru katika kuondoa marufuku ya uvunaji miti katika misitu ya kaunti ya Nyandarua, ambayo alisema imeathiri vibaya uchumi wa eneo hilo.

Alipuuzilia mbali mfumo wa kujenga uchumi kutoka chini kuelekea juu wa mpinzani wake mkuu William Ruto akisema vijana wanahitaji kazi bora zaidi, wala si mikokoteni.

Pia aliahidi mabadiliko ya katiba ili kuhakikisha mgawao sawa wa rasilimali.

“Usawa umehakikishwa katika Katiba yetu lakini maelfu ya watoto kutoka Mkoa wa Kati wanaacha shule kwa kukosa karo kutokana na ukosefu wa usawa katika usambazaji wa rasilimali,” alisema Raila.

Raila aliandamana na Magavana Francis Kimemia (Nyandarua), Lee Kinyanjui (Nakuru) na aliyekuwa Mbunge wa Gatanga Peter Kenneth, miongoni mwa viongozi wengine.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke