Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raila aahidi vijana nafasi 4 katika Baraza la Mawaziri atakapoingia Ikulu

0fgjhs38754pclce3 Raila aahidi vijana nafasi 4 katika Baraza la Mawaziri atakapoingia Ikulu

Tue, 12 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Kinara wa upinzani Raila Odinga amewahakikishia wananchi kuwa uchaguzi wa urais wa 2022 utakuwa huru na wa haki.

Kiongozi huyo wa ODM alisema kujitolea kwake na kwa Rais Uhuru Kenyatta kutahakikisha amani inadumu wakati wote wa kupigwa kwa kura nchini.

"Ninaweza kuwahakikishia kuwa uchaguzi wa rais utakuwa huru na wa haki kwani mimi na Uhuru na tumejitolea kuikomboa nchi hii jinsi mababu zetu walitaka iwe," alisema.

Waziri mkuu huyo wa zamani aliwataka vijana wasiwe na wasiwasi juu ya uwezekano wa kurudiwa kwa ghasia za baada ya uchaguzi.

"Hakutakuwa na vurugu za baada ya uchaguzi," Raila alisema alipokutana na baadhi ya viongozi wa vijana kutoka Mlima Kenya katika Chuo Kikuu cha Nairobi.

Wakati wa hotuba yake, Raila alisema pia ipo haja ya kuhakikisha wanawake wanapata nyadhifa serikalini jinsi katiba inavyosema.

Mwanasiasa hiyo aliongeza kwamba licha ya mahakama kufutilia mbali mchakato wa BBI lazima suluhu lipatikane ili kukabiliana na swala la wanawake kudunishwa katika uongozi.

Raila aliongeza kuwa kando la hilo pia watu wanaoishi na ulemavu watawakilishwa katika nyadhifa za uongozi serikalini.

Kinara huyo wa ODM aliahuidi kuwatengea vijana nyadhifa nne katika baraza la mawaziri iwapo atachaguliwa kuwa rais wa tano wa taifa.

Kiongozi huyo alitaja wakati ambapo alikuwa Waziri Mkuu na kusema kwamba aliendesha kongamano la kuwajenga vijana akiongeza kwamba atakapongia uingozini hiyo bado itakuwa ajenda yake.

"Wakati nilikuwa waziri mkuu, nilikuwa na mikutano ya mazungumzo na wafanyabiashara na pia vijana. Tulikuwa tukiifanya mikutano kila baada ya miwezi minne ili tupate maoni kuhusu ni changamoto zipi wanapitia na ni kwa njia ipi matatizo hayo yanaweza kusuluhishwa," alisema Odinga.

"Kuhusu swala la nafasi za mawaziri kwa vijana… naweza kusema zitakuwa zaidi ya nne," akaongeza.

Aliahidi kuwa na vijana katika Wizara ya Mambo ya nje watahusika na maswala ya mambo ya nje kwa kuwa raia wengi wanaoishi nje ya nchi ni vijana.

Aliahidi kwamba katika afisi ya Wizara ya Mambo ya Nje itashikiliwa na kijana ambao watakuwa wakishughulikia ya nje kwani idadi kybwa ya wananchi wanaoishi nje ya taifa ni vijana.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke