Kiongozi wa Azimio la Umoja nchini Kenya, Raila Odinga amedai kuwa Rais wa sasa wa nchi hiyo, William Ruto yupo katika mkakati wa kulipiza kisasi kwa watu embao hawakumuunga mkono katika kinyang’anyiro cha urais wa Agosti 9 mwaka huu.
Kiongozi wa Azimio la Umoja nchini Kenya, Raila Odinga amedai kuwa Rais wa sasa wa nchi hiyo, William Ruto yupo katika mkakati wa kulipiza kisasi kwa watu embao hawakumuunga mkono katika kinyang’anyiro cha urais wa Agosti 9 mwaka huu. Odinga amesema Rutto amewalenga zaidi maofisa wakuu wanne wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Juliana Cherera, Francis Wanderi, Irene Masit na Justus Nyang’aya ambao walionyesha wazi kutoridhishwa na namna mchakato wa kutangazwa kwa kiongozi huyo ulivyofanyika.