Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raila Odinga atua ICC

Raila Odinga Kuchukuliwa Hatua Za Kisheria Kutoa Madai Ya Video Ya Siri Raila Odinga

Fri, 14 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muungano wa upinzani wa Azimio la Umoja nchini Kenya, umeiandikia barua mahakama ya kimataifa ya jinai ICC, kuitaka kuanzisha uchunguzi kuhusiana na hali ya kisiasa nchini Kenya.

Kwenye Barua iliyoandikwa na wakili Paul Mwangi kwa mahakama hiyo ya ICC, iliyo na makao yake mjini the Haque, muungano huo umenakili masuala kadhaa ikiwemo kulengwa kwa waandamanaji na maafisa wa ulinzi wa serikali..

Aidha barua hiyo imewataja maafisa kadhaa waku wa serikali kwa kuhusika na uhalifu huo akiwemo inspecta mkuu wa polisi Japheth Koome. Barua hiyo imewasilishwa chini ya kifungu cha 25 ya sheria za mahakama hiyo ya ICC

Uhalifu mwingine uliotajwa kwenye barua hiyo ni pamoja na kuwashambulia waandishi wa habari, kupora mali ya viongozi wa muungano huo mbali na kutisha maisha ya baadhi yao.

Azimio sasa imeomba ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa ICC kuanzisha uchunguzi.

Baada ya uchaguzi mkuu wa 2007, wanaisasa kadhaa akiwemo aliyekuwa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na rais wa sasa William Ruto walifikishwa mbele ya mahakama ya ICC kwa tuhuma za kuhusika na uhalifu wa kivita, kufuatia ghasia zilizoibuka baada ya uchaguzi na kusababisha vifo vya watu kadhaa na mali ya mamilioni kuporwa au kuharibiwa.

Kesi hizo zote hata hivyo zilitupiliwa mbali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live