Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raila Odinga asema hataki mambo ya BBI tena

021cca606b3a2fbc Raila Odinga asema hataki mambo ya BBI tena

Fri, 20 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Raila alikubali matokeo ya rufaa ya BBI na kusema ni wakati sasa atamatishe siasa za mswada huoAlisema atatafuta njia mbadala za kusuluhisha masuala ambayo yalikuwa yamelengwa na mswada huoKuanguka kwa BBI itakuwa pigo kwa Raila na mrengo wa handisheki kwenye safari ya kuelekea IkuluKinara wa ODM Raila Odinga amesema siasa za BBI sasa zimefika mwisho baada ya uamuzi wa majaji saba wa Mahakama ya Rufaa.

Raila alisema yeye na mrengo wake wa ODM wameamua 'kuendelea na maisha' na maisha baada ya uamuzi huo wa mahakama.

Kwenye taarifa, Raila alisema imefika wakati kila upande uliohusika kuamua hatua watakayochukua baada ya uamuzi wa Ijumaa Agosti 20.

"Sisi, kama tulivyosema hapo awali, tulikuwa tujihusishe kiasi cha haja. Lakini sasa tunahisi kuwa itabidi tuendelee na mengine," Raila alisema.

Alisema ni wazi kuwa masaibu ni mengi Kenya na kwa hivyo atatafuta njia mbadala za kutatua masuala yaliyokuwa yameangaziwa na BBI.

"Ni wakati tuyaangaliwa mambo kwa mtazamo mpya na kuanza ajenda ya kuhakikisha mambo yamekuwa sawa nchini. BBI haikuwa suluhu la mwisho ila safari ya kubadili mambo tu. Kwa hakika tutakabili mambo haya ndani ya miezi au miaka ijayo," aliongeza Raila

Taarifa ya Raila ilijiri baada ya hali kuonekana wazi kuwa majaji wa Mahakama ya Rufaa watatupa nje rufaa ya BBI.

Majaji hao saba waliskiza rufa hiyo Juni na kisha kuenda faraghani kuandika maamuzi yao yaliyosomwa Ijumaa Agosti.

Walitia doa BBI wakisema Rais Uhuru Kenyatta ndiye aliyeianzisha ambapo ni kinyume cha katiba.

Uamuzi huo wa BBI ulikuwa wimbo mtamu kwa maskio ya Naibu Rais William Ruto na wandani wake ambao wamekuwa wakipinga BBI.

Akiongea Karen, Ruto alikuwa amewasuta wakereketwa wa BBI akisema hawana namna kwani kifo cha BBI kimewasili.

"The Die is Cast. Hakuna vile wanaweza kurudisha haya maneno nyuma. Tumewaambia imefika kiwanga sasa Wakenya wameamua kabla ya kuongea mambo ya kubadilisha katiba, tutabanga kwanza vile tutabadilisha uchumi," alisema DP Ruto



Kabla ya kupanga vile viongozi wataopata vyeo, kwanza tutapanga vile Wakenya milioni mingi ambao hawana kazi watapata kazi. Kabla ya kupanga vile viongozi watagawana mamlaka tutapanga kwanza vile tutawasaidia wakulima, wafanyibishara ili waweze kujimudu," aliongeza.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke