Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raila Odinga apewa ulinzi wa maafisa wa GSU

D0e926b6caa2ac97 Raila Odinga apewa ulinzi wa maafisa wa GSU

Sun, 17 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Maafisa wa kikosi cha ulinzi wa watu mashuhuri GSU ndio sasa wanamlinda kinara wa ODM Raila Odinga.

Licha ya kuwa upinzani Raila anaonekana kufurahia matunda ya serikali kumzidi hata Naibu Rais ambaye amekuwa akilalamikia kutendewa isivyo na na serikali yake.

Maafisa wa GSU waliondolewa kutoka kikosi cha usalama kinacholinda makazi ya DP Ruto hatua iliyozua cheche kali kisiasaRaila alionekana akilindwa na maafisa hao wakati wa mkutano wake kaunti ya Isiolo Oktoba 16.

Hilo lilidhihirika wazi wakati wa mkutano wa Azimio la Umoja na viongozi kaunti ya Isiolo Jumamosi Oktoba 17.

Maafisa wa GSU walionekana kwenye jukwaa huku wakiwa ngangari kuhakikisha kiongozi huyo wa upinzani yuko salama.

Baada ya vijana kuanza kuzusha wakimzomea Gavana Mohammed Kuti na kuendelea kusonga kwenye jukwaa maafisa hao walishika bunduki imara na kuhakikisha umati huo haujamfikia Raila.

Ni wazi sasa kuwa Raila anafurahia matunda ya serikali kikamilifu licha ya kuwa katika upinzani.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke