Serikali imeondoa Walinzi wote wa Kiongozi wa Upinzani, #RailaOdinga muda mfupi baada kuwatangazia Wananchi wajiandae kwa Maandamano ya Kimapinduzi kuanzia Julai 19, 2023, Maandamano ambayo yamepata kibali cha Mahakama
Uamuzi huo unakuja muda mfupi baada ya Odinga kutangazia Wananchi kuwa wajiandae kwa Maandamano ya Kimapinduzi kuanzia Julai 19, Maandamano ambayo yamepata pia kibali cha Mahakama.
Kwa mujibu wa taarifa, Askari 10 wanaomlinda Odinga na wengine wanaolinda Makazi yake jijini Nairoi, Kisumu na Siaya wameondolewa pamoja na Walinzi wanaowalinda Wabunge zaidi ya 50 wa Upinzani.
Wengine waliofutiwa Ulinzi ni Mwanasiasa Kalonzo Musyoka na Magavana Wanne. Leo Julai 17, 2023 Mahakama Kuu imefutilia mbali ombi la zuio la Maandamano hayo na kueleza kuwa ni Haki ya Kikatiba.