Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raila Odinga amtaka Chebukati ajiuzulu

Odinga Kenya Kmll Raila Odinga amtaka Chebukati ajiuzulu

Thu, 25 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa mgombea urais wa tiketi ya Azimio la Umoja, Raila Odinga jana Agosti 24,2022 amesema Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ya Kenya, Wafula Chebukati anatakiwa kujiuzulu kusimamia uchaguzi mdogo wa Kaunti za Mombasa na Kakamega kutokana na kushindwa kuendesha vizuri Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9,2022 nchini humo.

Odinga ambaye kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na Chebukati, Agosti 15, 2022 alishika nafasi ya pili kwa kupata kura milioni 6.9 nyumba ya William Ruto aliyepata kura milioni 7.1

Waziri mkuu mstaafu huyo amesema hayo wakati akizungumza na Wajumbe wa Azimio la Umoja kwenye ziara yake ya Mombasa inayolenga kumnadi mgombea ugavana wa Azimio la Umoja, AbdulSwamad Nassir.

"Wafula Chebukati aliwafanyia vitendo visivyo vya kiungwana makamishna wake waliokataa kusimama upande usio wa kweli, alipewa rushwa. Inatakiwa ajitoe kusimamia uchaguzi wa hapa Mombasa kwasababu amekosa sifa na Imani ya watu," Raila amemtuhumu Chebukati.

Hata hivyo, Odinga ametaja kusogezwa mbele kwa uchaguzi wa Kaunti mbili za nchi hiyo Kama hofu waliyonayo wapinzani wake juu ya Azimio la Umoja

"Nimeamua leo nije tuonane ana kwa ana kwasababu wamewanyima haki yenu ya msingi mara mbili kwa sababu tu ya uoga wao kuwa tutawashinda, nataka niwahakikishie tu haijalishi Mara ngapi watasogeza mbele kwenye kaunti ya Kakamega na Mombasa lakini tutawashinda tu," amesema.

Odinga ameendelea kusisitiza kuwa uchaguzi uliofanyika Agosti 9,2022 walishinda na IEBC haikutenda haki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: