Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raia wa Uganda mwenye umri wa miaka 70 ajifungua mapacha

Raia Wa Uganda Mwenye Umri Wa Miaka 70 Ajifungua Mapacha Raia wa Uganda mwenye umri wa miaka 70 ajifungua mapacha

Thu, 30 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Mwanamke wa Uganda mwenye umri wa miaka 70 amepata mapacha baada ya kupata ujauzito kupitia matibabu ya kupandikiza (IVF), na kuwa mwanamke mzee zaidi barani Afrika kujifungua, kwa mujibu wa hospitali alikopata watoto.

Kituo cha Kimataifa cha Hospitali ya Wanawake na Kituo cha Uzazi katika mji mkuu wa Uganda, Kampala, kilisema Safina Namukwaya alijifungua mtoto wa kike na wa kiume.

"Hadithi hii haihusu tu mafanikio ya matibabu; inahusu nguvu na uthabiti wa roho ya mwanadamu," hospitali hiyo ilisema kwenye Facebook, kufuatia Bi Namukwaya kujifungua kwa njia ya upasuaji Jumatano.

Bi Namukwaya alikiambia kituo cha binafsi cha NTV kwamba ilikuwa uzao wa pili katika miaka mitatu, baada ya kujifungua mtoto wa kike mnamo 2020.

Aliongeza kuwa alipata matatizo mengi wakati wa ujauzito, ikiwa ni pamoja na kutengwa na baba wa watoto.

“Wanaume hawapendi kuambiwa umebeba zaidi ya mtoto mmoja, tangu nilipolazwa hapa hajawahi kufika,” alisema.

Bi Namukwaya alisema hajui atawezaje kuwalea watoto hao, lakini anafurahi kuwa nao baada ya miaka mingi ya kuvumilia unyanyapaa na kejeli kwa kukosa watoto.

Chanzo: Bbc