Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raia wa Uganda aliyefichua ukatili wa Idi Amin apewa heshima za mwisho

Raia Wa Uganda Aliyefichua Ukatili Wa Idi Amin Apewa Heshima Za Mwisho Raia wa Uganda aliyefichua ukatili wa Idi Amin apewa heshima za mwisho

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Raia wa Uganda wamekuwa wakitoa heshima zao kwa waziri wa zamani katika serikali ya Idi Amin, Henry Kyemba, aliyefariki siku ya Alhamisi kutokana na matatizo yanayohusiana na kisukari akiwa na umri wa miaka 84.

Anaelezewa kuwa gwiji katika maisha ya wengi nchini Uganda, akihudumu katika nyadhifa tofauti katika serikali za Amin na Milton Obote, pamoja na Rais wa sasa Yoweri Museveni.

Alipokuwa akisimulia vyombo vya habari vya wakati wake kama msaidizi wa Obote, alisema aliwahi kuchukua risasi ambayo ilikusudiwa kumuua rais.

Pia anajulikana sana kwa kitabu chake, State of Blood: The Inside Story of Idi Amin, alichoandika baada ya kukimbilia uhamishoni mwaka 1977 alipokuwa akihudumu chini ya dikteta.

Kitabu hicho kilieleza kwa kina masimulizi ya moja kwa moja ya uzoefu wakati wa serikali ya kikatili ya Amin, kikifichua ukatili na ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na utawala huo.

Gazeti la kila siku linalomilikiwa na serikali, The New Vision, linasema kazi yake inachukuliwa kuwa hati muhimu ya kihistoria inayotoa "ufahamu wa kipindi cha giza katika historia ya Uganda".

Kyemba alirejea Uganda mwaka 1986, muda mrefu baada ya Amin kuondolewa madarakani mwaka 1979, na kutwaliwa na rais wa sasa.

"Nasikitika kwa kifo cha Henry Kyemba. Alikuwa gwiji katika maisha ya raia wa Uganda: mshauri wa marais Obote na Amin; mtumishi wa serikali aliyejitolea; mkosoaji jasiri wa ukatili wa Amin; mtunza kumbukumbu," Derek R Peterson, mwanahistoria wa Marekani aliyebobea katika historia ya kitamaduni ya Afrika Mashariki alisema kwenye mtandao wa X.

Naibu spika wa bunge la Uganda Thomas Tayebwa alimtaja Kyemba kama "mwanasiasa mashuhuri" ambaye alihudumu katika serikali tofauti "bila doa".

"Anaacha nyuma moja ya urithi unaorufahiwa ambao nchi hii itakuwa nao milele. Pumzika kwa Amani kiongozi," aliongeza.

Chanzo: Bbc