Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raia wa SA wanaopigana Israel watakamatwa - waziri

Raia Wa SA Wanaopigana Israel Watakamatwa   Waziri Raia wa SA wanaopigana Israel watakamatwa - waziri

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Waziri wa Mambo ya nje wa Afrika Kusini Naledi Pandor amesema kuwa raia wa taifa hilo wanaopigania Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) huko Gaza watakamatwa watakaporejea nchini humo, shirika la habari la AP linaripoti.

“Tayari nimeshatoa taarifa ya kuwatahadharisha wale ambao ni wa Afrika Kusini na wanapigana... Tuko tayari.

Ukirudi nyumbani, tutakukamata,” alinukuliwa akiambia hafla ya mshikamano wa Wapalestina mapema wiki hii.Haijabainika ni watu wangapi hatua hii inaweza kuathiri.

Afrika Kusini tayari ilikuwa imeonya mwaka jana kwamba raia wake wanaweza kushtakiwa ikiwa watapigana na IDF.

Gazeti la Haaretz Jumatano lilinukuu taarifa ya kijeshi ikisema kwamba "IDF inafanya kazi ili kutoa jibu kwa hatari zinazowezekana za usalama na kisheria wakati wanajeshi wanasafiri nje ya nchi.

IDF inafuatilia suala hilo kwa msingi unaoendelea, kwa uratibu na ushirikiano na serikali inayohusika au wizara.

”Afrika Kusini imekuwa mstari wa mbele katika upinzani wa kidiplomasia dhidi ya vita vya Israel huko Gaza, ambavyo vilichochewa na mauaji ya zaidi ya watu 1,200 na utekaji nyara wa wengine zaidi ya 200 mwezi Oktoba.I

lianzisha kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki kuzingatia iwapo Israel inatekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina huko Gaza.

Chanzo: Bbc