Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raia wa Nigeria wakasirishwa na ndege mpya ya rais

Raia Wa Nigeria Wakasirishwa Na Ndege Mpya Ya Rais.png Raia wa Nigeria wakasirishwa na ndege mpya ya rais

Thu, 22 Aug 2024 Chanzo: Bbc

Raia wengi wa Nigeria wameghadhabika baada ya ndege mpya kununuliwa kwa ajili ya Rais Bola Tinubu wakati ambapo uchumi unakumbwa na mzozo mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika kizazi.

Ndege hiyo imenunuliwa wiki mbili baada ya maelfu ya watu kumiminika barabarani kote nchini kulalamikia njaa inayoongezeka na kupanda kwa gharama ya maisha.

Bw Tinubu ambaye alichaguliwa mwaka jana kuongoza nchi yenye watu wengi zaidi barani Afrika, ameanzisha mageuzi kadhaa ya kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kuondolewa kwa ruzuku ya mafuta, ambayo imechangia mfumuko mkubwa wa bei, ambao kwa sasa ni zaidi ya 30%.

Rais Tinubu alisema mageuzi hayo ni muhimu ili kupunguza matumizi ya serikali na kuchochea ukuaji wa muda mrefu.

Mnamo Januari, rais wa Nigeria alitangaza kupunguza kwa asilimia 60 ya idadi ya maafisa wa serikali wanaosafiri nje ya nchi , ikiwa ni pamoja na wasaidizi wake mwenyewe.

Hata hivyo Jumatatu, rais aliondoka kuelekea Ufaransa kwa kutumia ndege mpya aina ya Airbus A330, ambayo imekuwa nyongeza ya hivi punde zaidi ya ndege zaidi ya tano za rais.

Gharama ya ndege hiyo haijawekwa wazi, na wala sababu ya safari yake hhaijaelezwa wazi.

Mtumiaji wa X @Fdmlearn alisema haikuwa sawa kwamba Wanigeria waliambiwa wapate maumivu ya kiuchumi wakati serikali inamnunulia rais ndege mpya.

Mtumiaji mwingine wa X @RealOlaudah alikasirika zaidi.

“Tuambizane ukweli. Ununuzi mpya wa ndege ya rais wa Airbus ya Tinubu kwa fedha za Nigeria bilioni 150 wakati wa njaa, na mahitaji ya kitaifa unaonyesha jinsi alivyo muovu, mbinafsi, mwenye kujifurahisha, na asiyejali masaibu ya Mnigeria wa kawaida.

Hata hivyo, @Timi_The_Law anasema anaunga mkono uamuzi wa rais kwani ndege hiyo si ya kibinafsi bali ni ya ofisi ya rais.

Chanzo: Bbc