Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raia wa Namibia wapinga Bunge kupokea msaada wa Dola Bilioni 1

Protest Namibia Raia wa Namibia waandamana nje ya Bunge kupinga faini Mauaji ya Ujerumani

Wed, 22 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waandamanaji 300 wamevamia Bunge lilipokuwa likijianda kupitisha msaada wa dola bilioni 1 toka kwa Ujerumani, wakisema kiwango hicho cha fidia ni kidogo sana.

Mei 28, 2021 Viongozi wa Namibia walitangaza kuwa Ujerumani imekubali kufadhili Miradi kwa kutoa msaada wa Dola bilioni 1 (sawa na Tsh. Trilioni 2.3) kufidia kilichotokea Kipindi cha Ukoloni.



Nae Waziri wa Ulinzi wa nchini humo, Frans Kapofi amesoma taarifa ya makubaliano hayo mbele ya Bunge huku akiitaja hatua hiyo kama mafanikio makubwa kwa Serikali kwa kuifanya Ujerumani kukubali kuchukua jukumu la kulipa fedha hizo kufuatia mauaji hayo.



Baadhi ya wanachi wa Namibia wakiwa nchini Ujerumani wakitazama masalia ya watu waliouwa katika mauaji ya kimbari.

Aidha, Ujerumani iliomba msamaha Namibia kutokana na Mauaji ya Kimbari ya Kabila la Herero na Nama yaliyofanyika 1904 na 1908 ambapo pia walipora mali za Wanamibia

Chanzo: www.tanzaniaweb.live