Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raia wa Marekani afikishwa kortini kwa mashtaka ya kuwabaka watoto

Kenya High Court Raia wa Marekani afikishwa kortini kwa mashtaka ya kuwabaka watoto

Tue, 21 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Raia mmoja wa Marekani anayeishi nchini Kenya, na ambaye alikuwa ameachiliwa huru kutoka gerezani baada ya kupatikana na hatia ya ubakaji wa watoto, leo amefikishwa na kufunguliwa mashtaka mapya ya ubakaji.

Terry Ray, aliachiliwa huru miezi mitatu iliyopita kwa misingi isiyofahamika licha ya kuwa alikuwa akitumikia kifungo cha miaka hamsini gerezani.

Mshukiwa huyo amekuwa akizuiliwa chini ya ulinzi mkali tangu tarehe kumi mwezi huu, alifikishwa mahakamani huku ulinzi ukiimarishwa nje na ndani ya mahakama hiyo viungani mwa mji mkuu Nairobi.

Kriieger alifikishwa mbele ya hakimu mkuu mkaazi wa Mavoko Barbra Ojoo na kusomewa mashtaka ya ubakaji.

Mshukiwa huyo alimfahamisha hakimu kuwa hakuelewa ni kwa nini wakili wake hakufika mahakamani na juhudi zake za kutaka kuachiliwa kwa dhamana zilikataliwa na jaji .

Upande wa mashtaka uliiambia mahakama kuwa endapo mshukiwa huyo ataachiliwa kwa dhamana, basi huenda akatoroka nchini kwa kuwa ni raia wa Marekani.

Hakimu huyo alisema mshukiwa huyo huenda akahukumiwa kifungo cha miaka mitano ikiwa atapatikana na hatia na kuwa hajapewa ushahidi wowote kubainisha ikiwa mshukiwa huyo anastahili matibabu maalum na hivyo hamna sababu ya kuachiliwa kwa dhamana.

Mahakama hiyo ilifahamishwa kuwa Krieger anakabiliwa na mashtaka mengine ya kiuhalifu nchini Marekani.

Krieger alihukumiwa kifungo cha miaka hamsini gerezani mwaka wa 2014 baada ya kukiri mashtaka ya kuhusika na kashfa ya kunasa picha za ponografia za watoto.

mwaka wa 2022 aliachiliwa huru kwa misingi isiyojulikana baada ya kuhudumu miaka minane pekee.

Chanzo: Bbc