Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raia wa Mali wanapiga kura siku ya Jumapili

Raia Wa Mali Wanapiga Kura Siku Ya Jumapili Raia wa Mali wanapiga kura siku ya Jumapili

Fri, 16 Jun 2023 Chanzo: Voa

Uchaguzi huo ni wa kwanza kuandaliwa na jeshi, tangu ilipotwaa madaraka mwezi Agosti 2020 katika nchi iliyokumbwa na mgogoro wa kisiasa, usalama, na kiuchumi. Matatizo hayo bado hayajatatuliwa kwa kiasi kikubwa ikimaanisha kwamba kura hiyo inaweza kuvurugwa

Raia wa Mali wanapiga kura siku ya Jumapili kufanya maamuzi juu ya katiba ya jeshi linalotawala, ambayo imechochea uvumi kwamba mtawala mwenye nguvu wa nchi hiyo atawania katika uchaguzi.

Uchaguzi huo ni wa kwanza kuandaliwa na jeshi, tangu ilipotwaa madaraka mwezi Agosti 2020 katika nchi iliyokumbwa na mgogoro wa kisiasa, usalama, na kiuchumi. Matatizo hayo bado hayajatatuliwa kwa kiasi kikubwa ikimaanisha kwamba kura hiyo inaweza kuvurugwa. Ni hatua muhimu katika njia ya kuurudisha utawala wa kiraia hapo Machi 2024, chini ya ahadi zilizotolewa na jeshi lenyewe.

Lakini chini ya miezi tisa kabla ya tarehe ya mwisho, Mali haina uwazi juu ya jukumu la baadaye la jeshi, ikiwa ni pamoja na kiongozi wa kijeshi Kanali Assimi Goita. Raia wa Mali watapiga kura juu ya rasimu ya katiba kuanzia saa mbili kamili asubuhi kwa saa za huko siku ya Jumapili, kukiwa na masanduku ya kura yenye rangi ya kijani ikimaanisha NDIYO, na rangi nyekundu ikimaanisha kura za HAPANA.

Matokeo yanatarajiwa kutolewa ndani ya masaa 72. Serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa katika mageuzi hayo. Inadai kurekebisha katiba ya sasa ya nchi hiyo, iliyotungwa mwaka 1992 na mara kwa mara inalaumiwa kwa matatizo yanayotokea Mali.

Chanzo: Voa