Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raia wa Liberia wanapiga kura kumchagua rais na wabunge

Raia Wa Liberia Wanapiga Kura Kumchagua Rais Na Wabunge Raia wa Liberia wanapiga kura kumchagua rais na wabunge

Tue, 10 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Wagombea 19 wanatumai kuchukua nafasi ya aliyemaliza muda wake, nyota wa zamani wa soka George Weah, ambaye anawania muhula wa pili.

Wapinzani wakuu wawili ni makamu wa rais wa zamani Joseph Boakai na mfanyabiashara Alexander Cummings.

Wote walikuwa katika muungano wa vyama vya upinzani lakini muungano huo ulivunjika baada ya kutofautiana kuhusu nani anayefaa kugombea urais.

Licha ya maendeleo kadhaa katika suala la elimu na usambazaji wa umeme, wakosoaji wanasema kumekuwa na ufisadi mkubwa wakati wa Bw Weah mamlakani.

Anaahidi kujenga barabara mpya, suala muhimu linalokuja wakati unaofaa wakati wa uchaguzi katika msimu wa mvua wakati sehemu kubwa ya barabara za kuelekea mji mkuu Monrovia zikiwa hazipitiki.

Bw Weah aliingia mamlakani mwaka wa 2017 alipoungwa mkono na watu wengi baada ya majaribio mawili ya hapo ya awali yakuwania kiti cha urais bila mafanikio.

Chanzo: Bbc