Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raia wa Guinea afariki kituo cha wahamiaji Mülheim

Polisii Ms Raia wa Guinea afariki kituo cha wahamiaji Mülheim

Mon, 8 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Gari ya polisi nje ya kituo cha wahamiaji mjini Mülheim ambako mwanamume wa Guinea alifariki kufuatia operesheni ya polisi.

Mwanamume wa umri wa miaka 26 raia wa Guinea amekufa baada ya kukabiliana na maafisa wa polisi katika kituo cha kuwapokea wahamiaji katika mji wa Mülheim magharibi ya Ujerumani.

Polisi wameitwa katika kituo hicho na wakala wa usalama uliosema mwanamume huyo alikuwa amewashambulia maafisa wake. Wakati polisi walipowasili mwanamume huyo alikuwa chumbani kwake na akawashambulia.

Kwa mujibu wa ripoti ya polisi walijaribu mara mbili kumdhibiti wakati walipomkimbiza katika kituo hicho. Baadaye walifanikiwa baada ya maafisa wawili kuumwa na afisa mwanamke kupigwa kichwani.

Magari ya kubebea wagonjwa yaliitwa kusaidia wakaazi na maafisa hao wawili. Mhamiaji huyo wa Guinea alipoteza fahamu alipokuwa akitibiwa ndani ya gari la wagonjwa na baadaye kupelekwa hospitali ambako alifariki dinia.

Polisi katika mji jirani wa Bochum wanafanya uchunguzi wa mauaji kama utaratibu wa kawaida wakisubiri ripoti ya uchunguzi wa daktari. Maafisa waliohusika katika tukio hilo wanapewa ushauri nasaha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live