Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raia wa Afrika Magharibi wapuuza kupata chanjo ya COVID-19

QQEWTWE Raia wa Afrika Magharibi wapuuzia kupata chanjo ya COVID-19

Mon, 15 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chanjo za kuzuia Covid-19 sasa zinapatikana kwa wingi barani Afrika; ni asilimia 5.7 tu ya watu wamekamilisha ratiba kamili ya chanjo, kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO). Nchini Benin au Senegal, kwa mfano, raia wanasita kupewa chanjo.

Mwezi mmoja uliopita, Baraza la Mawaziri la Benin liliamua kuendeleza hatua za vizuizi zilizohusishwa na Covid-19, kama kiwango cha chanjo katika ngazi ya kitaifa kitakuwa hakijaboreshwa. Kulingana na takwimu rasmi, nchi hiyo imerekodi chini ya kesi 25,000 zilizothibitishwa za maambukizi ya virusi vya Corona kwa jumla, pamoja na vifo 161. Mwanzoni mwa wiki iliyopita, kiwango cha chanjo hakikufikia 4%.

"Bado nina mashaka"

Katika mitaa ya Cotonou, baadhi ya raia bado anasita kupewa chanjo, amebainisha mwandishi wetu maalum huko Cotonou, Magali Lagrange. Watu wachache wanasubiri mbele ya chumba kwenye kituo cha afya, ambapo watapata chanjo dhidi ya virusi vya corona.

Wagonjwa hupewa hati ya taarifa ... kabla ya kuchomwa sindano. Hervé anakiri kwamba alisi kupwa chanjo: “Niliamua, baada ya muda, kupata chanjo ili kutoa mchango wangu na hasa kwamba nina wazazi wazee tunaoishi nao pamoja. Kwa kile tulichosikia kwenye mitandao ya kijamii, inatufanya kusita kidogo. "

Chanzo: www.tanzaniaweb.live