Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raia mwingine auawa katika maandamano ya Khartoum

Khartoum Aaa.jpeg Raia mwingine auawa katika maandamano ya Khartoum

Mon, 31 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwandamanaji mmoja ameuawa siku ya Jumapili wakati vikosi vya usalama vya Sudan vilipokabiliana na maelfu ya raia wanaoendelea kupinga utawala wa kijeshi nchini humo katika maandamano ya Khartoum na miji mingine.

Tume ya madaktari wa Sudan imethibitisha juu ya kifo cha mwandamanaji mmoja aliyekuwa na umri wa miaka 27 na kwamba aliuawa mjini Khartoum akiwa na jeraha kifuani. Waandamanaji kadhaa walionekana wakipata shida ya kupumua na kuvuja damu baada ya kupigwa na mabomu ya kutoa machozi. Takriban watu 79 wameuawa na mamia kujeruhiwa katika msako wa maandamano ya kupinga mapinduzi, kulingana na kundi huru la madaktari.

Maandamano ya Jumapili pia yalifanyika katika maeneo mengine yakiwemo miji ya kaskazini ya Atbara na Dongola, na huko Darfur magharibi mwa nchi. Mjini Khartoum, vikosi vya usalama vilifunga madaraja muhimu na barabara zinazoelekea kwenye ikulu ya rais. Kulingana na wanaharakati, watu takribani 45 walikamatwa na mamlaka kabla ya maandamano ya Jumapili.

Mamlaka za Sudan mara kwa mara zimekanusha kutumia risasi za moto dhidi ya waandamanaji, na kusisitiza kuwa maafisa wengi wa usalama wamejeruhiwa. Jenerali mmoja wa polisi aliuawa kwa kuchomwa kisu wakati wa machafuko hayo mapema mwezi huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live