Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raia, Polisi wauawa katika shambulio la risasi

Image 222 1140x640.png Raia, Polisi wauawa katika shambulio la risasi

Thu, 22 Dec 2022 Chanzo: dar24.com

Watu watatu raia wa Kenya, wakiwemo Polisi wawili wameuawa katika shambulio la wanamgambo wa al-Shabab lililofanyika kaskazini mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa tarifa ya Polisi nchini humo, imeeleza kuwa tayari imeanza kuwasaka washambuliaji pamoja na maafisa wengine waliojisalimisha wakati wa tukio hilo.

Mkuu wa Polisi, George Seda amesema waliouawa walikuwa kwenye gari la Polisi eneo la kati la Kambi ya Hayley Lapsset na mji wa Garissa, lililopo kaskazini mashariki karibu na mpaka na nchi ya Somalia.

Kundi la kigaidi la Al-Shabab la nchini Somalia ambalo ni washirika wa al-Qaida, wanashukiwa kutekeleza shambulio hilo ingawa bado halijathibitisha rasmia.

Chanzo: dar24.com