Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raia 2 wa Nigeria waaga dunia wakijivinjari Kilimani, wanawake 2 watiwa mbaroni

Bcc2ce9210af2d52 Raia 2 wa Nigeria waaga dunia wakijivinjari Kilimani, wanawake 2 watiwa mbaroni

Sun, 11 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Raia wawili wa Nigeria walifariki dunia baada ya kujivinjari na marafiki zao usikuJamaa mmoja anasemekana aliruka kutoka orofa ya saba na mwengine naye alizirai akiwapikia wageniWanawake watatu wenye kati ya umri wa miaka 23 na 25 wamekamatwa huku polisi wakianzisha uchunguzi wa kilichotokea usiku huoPolisi wanachunguza kisa ambapo jamaa mwenye umri wa miaka 23 raia wa Nigeria kwa jina Ademuajiami Courage Maxwell aliruka kutoka orofa ya saba ya jumba la Skyhorse mtaani Kilimani.

Maafisa wa polisi pia walipata dawa za kulevya katika nyumba hiyo na wameanzisha uchunguzi kubaini kilichotokea usiku huo.

"Kuna mmoja ambaye alifariki dunia mapema ambaye inaaminika aliruka kutoka orofa ya saba ya nyumba hiyo. Pia tulipata dawa za kulevya katika nyumba hiyo," alisema OCPD wa Kilimani Muturi Mbogo.

Hata hivyo, jamaa huyo na marafiki zake walikuwa wamekusanyika usiku uliotangulia kujivinjari.



Read also

Naibu Rais Atoklezea Amevalia Rangi ya Chama cha Chungwa

"Walikuwa wakipiga kelele. Nilikuja nikazima stima. Walikuja wakanisihi niziwashe wakiahidi kutopiga kelele, niliziwasha tena. Baada ya hapo mimi niliondooka," keyateka alisema.

Kulingana na walioshuhudia kisa hicho, jamaa wa pili Mnigeria ambaye bado hajatambulika alikuwa jikoni akiwapikia wageni zaidi ya 20 waalikwa.

Hata hivyo alizirai na kufariki dunua kabla ya ambulansi kufika na kumkimbiza hospitalini.

"Bado hatujafanya upasuaji kuabini kilichomuua," OCPD aliongeza.

Kulingana na maafisa, ni watu watano tu walikuwa katika eneo la tukio walipowasili na wanawake watatu walitiwa mbaroni.

Wanawake hao ni Verah Osebe, Anastheni Manji na Diana Moraa ambao wanaripotiwa kuwa kati ya umri wa miaka 22 na 25.

Jamaa mwingine kutoka Nigeria kwa jina Kebor Kamar Omar ambaye alikuwa miongoni mwa wanaume hao alizimia na kukimbizwa hospitalini.



Read also

Mke wa Afisa Aliyemalizwa na Kangogo Asema Mshukiwa Alitaka Kukutana na Watoto Wao

Alitibiwa na kuruhusiwa kuelekea nyumbani.

Siku moja iliyopita TUKO.co.ke iliripoti kuwa mhudumu wa baa aliaga dunia baada ya kufumaniwa akiuza vileo usiku.

Carolyne Achieng anasemekana alizirai katika kituo cha biashara cha Laknyiro katika kata ya Gwasi eneo bunge la Suba Kusini kaunti ya Homa bay wakati polisi walipomshambulia mahali pa kazi.

Maafisa wa polisi kutoka Kituo cha Polisi cha Magunga walikuwa wamepokea habari kwamba baa hiyo ilikuwa ikiendelea kuhudumu nyakati za kafyu na waliamua kuvamia mahali hapo saa mojajioni.

Achieng na mhudumu mwingine mmoja waliamriwa kupakia kreti za pombe zitakazotumiwa kortini kama ushahidi kwamba wanakiuka amri za kutotoka nje.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke