Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RSF yatuhumiwa kufanya mauaji ya halaiki Sudan

RSF Yapinga Mpango Wa Msaada Uliyofikiwa Kati Ya Jeshi La Sudan Na UN RSF yatuhumiwa kufanya mauaji ya halaiki Sudan

Mon, 8 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashirika ya kiiraia na ya matibabu ya Sudan yamevituhumu Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) kuwa vimwefanya mauaji 3 ya halaiki ndani ya siku mbili, ambayo yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 68 na mamia kujeruhiwa katika mashambulizi yaliyolenga majimbo ya Al-Jazira, Darfur Kaskazini na Kordofan Kusini, sambamba na uporaji wa mali ya umma.

Kamati ya Jumuiya ya Madaktari ya Sudan imesema kuwa, watu 28 waliuawa na wengine 240 kujeruhiwa katika kijiji cha Umm Adham, eneo la Al-Hasahisa, katika jimbo la Al-Jazeera katikati mwa Sudan, katika shambulio la RSF, Jumamosi iliyopita.

Kamati hiyo imeeleza katika taarifa yake kwamba kikosi cha Rapid Support Forces "kilifanya shambulizi kwa kutumia silaha nzito na nyepesi kwenye kijiji hicho, baada ya kukizingira na kuwafyatulia risasi ovyo wakazi wake, hali iliyopelekea idadi hiyo kubwa ya watu kujeruhiwa."

Kamati hiyo imesema ni vigumu kujua idadi kamili ya wahanga wa shambulizi hilo “kutokana na kutoweza kufika kwenye vituo vya afya huku kukiwa na ufyatulianaji wa risasi, kukatwa huduma ya mawasiliano, hali ya hofu na kuhama kwa wakazi wa kijiji hicho.” Mamilioni ya watu wamekiimbia makazi yao Sudan kutokana na vita

Kamati hiyo imetoa wito kwa jamii ya kimataifa na mashirika yote ya kutetea haki za binadamu "kuingilia kati mara moja kukomesha uhalifu huo na kufanya kazi kuwawajibisha waliohusika na mauaji haya."

Kwa upande wake, "makundi ya upinzani" katika mji wa Al-Hasahisa katika Jimbo la Al-Jazeera yamevituhumu Vikosi vya Msaada wa Haraka kuua zaidi ya watu 20 na kujeruhi wengine 200 "katika mashambulizi yanayoendelea tangu siku ya Jumamosi.

Katika jimbo la Darfur pia, Harakati ya Haki na Usawa, inayoongozwa na Jibril Ibrahim, imewashutumu wapiganaji wa RSF kuwa wameua raia 20 na kuwajeruhi makumi ya wengine, wengi wao wakiwa wachungaji katika vijiji vya magharibi mwa mji wa El Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini.

Harakati hiyo imeuomba Umoja wa Mataifa na jamii ya kimataifa kuilazimisha RSF kuheshimu mikataba na sheria za kimataifa za haki za binadamu, na kuwawajibisha wapiganaji wake kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live