Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RSF yapinga mpango wa msaada uliyofikiwa kati ya jeshi la Sudan na UN

RSF Yapinga Mpango Wa Msaada Uliyofikiwa Kati Ya Jeshi La Sudan Na UN RSF yapinga mpango wa msaada uliyofikiwa kati ya jeshi la Sudan na UN

Fri, 22 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Wanamgambo wa RSF nchini Sudan wamekataa makubaliano kati ya serikali ya kijeshi ya nchi hiyo na mashirika ya Umoja wa Mataifa ya kupeleka misaada ya kibinadamu katika eneo maskini la Darfur.

Siku ya Alhamisi, gavana wa Darfur Minni Minawi alitangaza kuwa amefikia makubaliano ya msaada kuwasilishwa eneo la magharibi kupitia njia mpya inayodhibitiwa na jeshi la Sudan.

Lakini RSF, ambayo inadhibiti sehemu kubwa ya Darfur, ilisema mashirika ya Umoja wa Mataifa hayajashauriana nayo kuhusu utoaji wa misaada.

Pia ilishutumu "utawala wa zamani wenye msimamo mkali" kwa kujaribu kusafirisha silaha hadi Darfur - madai ambayo serikali ya kijeshi haijajibu.

Maafisa wakuu wa Umoja wa Mataifa wamesema vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan ni "mojawapo ya jinamizi mbaya zaidi la kibinadamu katika historia ya hivi karibuni" na vinaweza kusababisha janga kubwa zaidi la njaa duniani.

Mwezi uliopita, Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) lilisema limeweza tu kufikisha misaada muhimu kwa 10% ya wale wanaohitaji katika maeneo yaliyokumbwa na vita, kama vile Darfur.

Mapambano haya yanatokana na masuala kama vile uporaji, vitisho vya usalama na vizuizi barabarani.

Chanzo: Bbc