Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RSF yaishutumu Kenya, Djibouti kwa kuchochea mgogoro Sudan

Mkuu Wa RSF Atoa Wito Kwa Jumuiya Ya Kimataifa Kuingilia Kati RSF yaishutumu Kenya, Djibouti kwa kuchochea mgogoro Sudan

Mon, 8 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hatua ya nchi nne za Afrika ya kumkaribisha mkuu wa Vikosi vya Msaada wa Haraka RSF vya nchini Sudan kuzitembelea nchi hizo, imeshadidisha mgogoro na vita vya uchu wa madaraka baina ya majenerali wa kijeshi nchini humo.

Tarehe 27 Disemba 2023, Mkuu wa Vikosi vya Msaada wa Haraka vya Sudan (RSF), Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo maarufu kwa jina la Hemedti alitembelea Uganda, siku iliyofuatia alielekea Ethiopia, tarehe 31 Disemba akafanya ziara nchini Djibouti na tarehe 3 mwezi huu wa Januari akatembelea Kenya na kuonana na Rais William Ruto wa nchi hiyo.

Shirika la habari la Tasnim limenukuu duru mbalimbali zikisema kuwa, ziara hiyo ya mzunguko ya mkuu wa vikosi vya RSF imeshadidisha mgogoro ndani ya Sudan kiasi kwamba serikali ya kijeshi ya nchi hiyo chini ya uongozi wa Jenerali Abdel Fattah al Burhan imechukua hatua kali dhidi ya nchi zilizompokea Dagalo ikiwa ni pamoja na kumwita nyumbani balozi wa Sudan aliyekuweko nchini Kenya. Majenerali wa kijeshi walioisabishia Sudan maafa makubwa

Ijapokuwa jeshi la Sudan chini ya Jenerali al Burhan ndilo linalodhibiti taasisi za serikali, Wizara ya Mambo ya Nje, taasisi za usalama za nchi hiyo pamoja na Jeshi la Anga, lakini uzoefu wa vita baina ya majenerali wa kijeshi vinavyoendelea kwa miezi 9 sasa huko Sudan unaonesha kuwa, vyombo na taasisi zote hizo zinazodhibitiwa na jeshi la Sudan zimeshindwa kufanya jambo la maana la kukabiliana na Vikosi vya Msaada wa Haraka.

Kabla ya hapo pia, mkuu wa serikali ya kijeshi ya Sudan, Jenerali Abdel Fattah Al-Burhan alikuwa amesema kwamba, jeshi lake litaendelea kupambana na wapiganaji wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) na hakuna mapatano yoyote yaliyofikiwa.

Al-Burhan alisema hayo katika hotuba yake ya kwa njia ya video iliyosambazwa Ijumaa kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Telegram na kusisitiza kwa kusema: "Hakuna maridhiano wala makubaliano tuliyofikia na waasi. Tutapigana hadi wanamgambo wakome, au sisi tukome."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live