Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RSF yadaiwa kukata mawasiliano kote Sudan

Sudan Mawasiliano Kote.jpeg RSF imekata mawasiliano kote Sudan

Sat, 10 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afisa wa huduma za mawasiliano wa Sudan amesema Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) ndivyo vinavyohusika na kukatika mawasiliano kote Sudan kwa siku ya nne mfululizo.

Mkurugenzi wa mtandao wa mawasiliano wa Zain-Sudan ambao ndio mtandao mkubwa zaidi wa mawasiliano nchini humo, Al-Fatih Orwa amesema kuwa, Rapid Support Forces (RSF) wamekata huduma za kampuni hiyo kwa kusimamisha jenereta za umeme katika kituo chake kikuu cha data eneo la Jabra mjini Khartoum, ambako kumesababisha kukatika kwa mawasiliano kote nchini Sudan.

Awali, waziri wa zamani wa mawasiliano, Hashem Hasab al-Rasoul, aliithibitishia televisheni ya Al Jazeera ya Qatar kwamba kilichotokea ni kufungwa kwa huduma za mawasiliano kwa maelekezo ya Kikosi cha Msaada wa Haraka kwa makampuni mbalimbali.

Amefafanua kuwa kufungwa kwa mawasiliano ya simu ya nchi nzima kwa sasa kumetumia kwa njia ile ile ambayo Serikali ilitumia hapo awali wakati wa matukio makubwa nchini Sudan.

Ameonya juu ya madhara ya "janga" la kusimamisha huduma ya mawasiliano kwa maisha ya Wasudani, kwa sababu kunavuruga uchumi na maisha ya watu kwa kusitisha huduma za benki.

Mitandao ya mawasiliano na intaneti ilisimamishwa kwa muda tangu Ijumaa wiki iliyopita katika majimbo mengi ya Sudan, kisha ikarejea tena kabla ya kukatwa kabisa Jumanne iliyopita, katika dhihirisho jipya la athari za vita na mapigano yanayoendelea nchini humo tangu Aprili mwaka jana kati ya jeshi la Serikali na Vikosi vya Msaada wa Haraka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live