Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RSF ya Sudan yaelezea mpango wake kumaliza vita

RSF SUDAN RSF ya Sudan yaelezea mpango wake kumaliza vita

Mon, 28 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha wapiganaji wanaopambana na jeshi la Sudan (RSF limetoa maoni yake kuhusu jinsi ya kumaliza mzozo kati yake na jeshi la kawaida la nchi hiyo, kuashiria kuwa tayari kwa suluhu iliyofikiwa.

Kiongozi wake, Luteni Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, anayejulikana pia kama Hemedti, alitoa taarifa ndefu kwenye X (zamani Twitter) mnamo tarehe 27 Agosti kuelezea "maono ya kikundi hicho kuhusu suluhu ya kina kumaliza vita na kujenga Sudan mpya".

Ilisema katika taarifa suluhu lolote la kumaliza vita "lazima liweke nchi kwenye njia ya utawala kamili wa kiraia unaozingatia kanuni za kidemokrasia".

Ilisema "suluhisho lazima lishughulikie vyanzo vya vita vya Sudan kupitia mazungumzo mapana na shirikishi yanayowashirikisha wadau wote wa kiraia" na "lazima ielekezwe katika kufikia usitishaji vita wa kudumu".

Iliongeza kuwa "jeshi jipya la kitaifa" lazima liundwe nchini Sudan.

Kauli hiyo ilitolewa siku hiyo hiyo ambayo kiongozi anayehudumu kama rais madarakani na mkuu wa majeshi wa Sudan, Luteni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, aliwasili katika mji wa mashariki wa Port Sudan.

Ilikuwa ni safari ya kwanza ya Jenerali Burhan katika mji huo, ambao umeepushwa na mapigano hadi sasa, tangu mzozo huo ulipozuka katikati ya mwezi wa Aprili.

Vyombo vya habari vya Sudan vimeripoti kuwa anatarajiwa kusafiri kwenda Misri na Saudi Arabia hivi karibuni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live